Msaada wa kisheria kwa huyu dada

Nyalotsi

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2011
Posts
6,986
Reaction score
5,058
Nina mpwa wangu kaolewa miaka mitano iliyopita. Kabla ya kuolewa alikuwa mfanyabiashara, na alipoolewa mumewe akamwambia afunge biashara yake wawe wanafanya pamoja akakubali.

Baada ya muda mumewe akaanza kumzuia kuingia dukani na kuweka wafanyakazi wa kuuza. Mke alipomuuliza aliishia kumfokea tuu na kumwambia ndugu zake wamemwambia anaiba hela. Baadaye akamwambia akae tuu nyumbani yeye si mwanamke?

Kinachosumbua ni kwamba sasa hivi hata nguo hamnunulii, vocha ndugu zake ndio wanamnunulia na mwanaume anaweza kuondoka bila kuaga zaidi ya miezi mitatu na asipige simu.

Alipoongea na ndugu wa upande wa kiume walimjibu vibaya kiasi cha kutaka kuondoka lakini hakuweza kufanya hivyo kwani wana watoto.

Kilichonifanya kuomba ushauri;

Ndugu zake tunataka kumpa mtaji ili afungue biashara yake ambayo itamsaidia kwenye mahitaji yake madogo madogo kwani hajazoea kukaa nyumbani.
Pia uhakika wa uhai wa mtu ni mdogo sana na mumewe anaweza kufa muda wowote mpwa akashindwa pa kuanzia kwani tuna uhakika ataporwa mali zote(japokuwa anaweza kutangulia yeye).

Ni taratibu zipi za kisheria au kijamii za kufuata?

Tukifanya hivyo ni kosa gani tutakuwa tumefanya?

Nitashukuru kama nitapewa na njia sahihi ya kupita.
 
Wandugu, hamna wenye utaalamu wa mambo haya?
 
Sheria za kimila zinazopingana na katiba za nchi si halali kwa mujibu wa utaratibu wa sheria za nchi.ibara ya 24 ya katiba ya tz inasema kila mtu anayo haki ya kumiliki mali,ibara ya 13(1)Watu wote sawa mbele ya sheria na wanayo haki bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheriag .hivyo sheria ya kumwambia yeye ni mwanamke tu akae nyumbani imepitwa na wakati kwani inapingana na katiba ya tz inayosema watu wote ni sawa. pia sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kifungu 59 nacho kinampa mwandoa
 
Pia sheria ya ndoa inatambua kuwa mali iliyopatikana kwa ushirikiano wa mume na mke wote wana haki sawa hata kama mwanamke alikuwa kazi yake kupika tu mfano kesi bi hawa mohamed zidi ya ally seif na hololia pastory zidi ya ephrem benaldo wanake hao walishinda kesi ambazo kesi zao zinafanana na ya dada yako. pia kumbuka mwanaume kuondoka bila kuaga na hakucha matumizi ni kosa kwa mujibu wa sheria ya ndoa ni kutelekeza familia.
 
Kama ndoa inahatarisha maisha bora ife. ila kuwa makini kaka usiwe chanzo cha kuvunja ndoa ya dada yako.
 
alfredy rafiki yangu sana huyu, haahah! Umeshawamaliza hapo, vile vitini nilivyokuuzia ni silaha tosha mzee ongeza pesa nikupe vingine mkuu
 
...Alfred umeeleza vizuri mkuu,
naomba niongeze na Mimi kidogo kwa ajili ya kumsaidia pa kuanzia.

hayo yote aliyoyaeleza kwa ufupi tuyaite mgogoro.

sasa kama Ni mgogoro, ushauri wangu sehemu ya yeye kuanzia kutatua mgogoro zipo nyingi, kwa kwa wanandugu, ambao tayari wameonesha kumkandamiza (upande WA mwanamume) hatua ya pili... Aende kwenye BARAZA LA USULULISHI WA NDOA (Marriage Concilliation Board) ambalo lipo Kila kata, aele hayo matatizo yake, then mwanamume aitwe.

PIA anaweza kwenda ustawi jamii, kwenda kuwasilisha malalamiko yake ya kutopata matunzo.

lakini kama ataona ndoa haina muelekeo (hasa baada ya kupeleka suala lake barazani na kushindikana) anaweza kudai talaka na kuomba kugawana Mali.

ambapo hapa sasa itabidi aende mahakamani tena baada ya kupata cheti cha kuvunjika kwa ndoa kutoka barazani.

asanteni
 
Kama ndoa inahatarisha maisha bora ife. ila kuwa makini kaka usiwe chanzo cha kuvunja ndoa ya dada yako.

lengo sio kuvunja ndoa yake, tunataka kumsaidia asiwe non productive and dependant. Ndio maana nauliza akipewa mtaji na ndugu zake italeta shida yoyote ya kisheria? asante kwa maelezo yako lakini.
 
Ishu ni kumpa mtaji huyo bidada?

Yes ndugu yangu. Unajua unapokuwa na ndugu ambaye unajua anaweza kutafuta hela ila anakatazwa na watu inauma sana. Ndugu yako ni ndugu yako tuu hata kama anaishi kwa watu wengine.

Take this too; your husband is not your relative. he is only your best friend and can change any time.
 

Inaonyesha kabisa kuwa mkimpa mtaji huyo ndugu yenu, mume wake atakuja kuharibu tu baadae, pengine anaweza fanya lolote mkawa kama mmetupa pesa. Mi ninachoona, kwanza hao wanandoa wapelekwe kwenye mabaraza ya usuluhishi huyo mume akaseme kinachomfanya yeye kufanya maamuzi ya ajabu ajabu... akitulia na kukubali mkewe kufanya kazi ni heri ila akiendelea na tabia zake unatafuta solution mbadala...
Point of correction, my husband is my enemy...
 
Kwa mambo yalivyo aidha mume aelimishwe kuhusu haki za mke ama mke aache ndoa na kufanya yake maana kama alivyopokwa mali zake hadi sasa kubaki nyumbani mkimsaidia tena atapokwa tena.
 
Mmh ushauri wanga, nend kweny haki za wanawake offis ziko kinondoni manyany watakusaidia xn,unatakiwa uend mapem,ni wanasheria wanawak wanaotetea haki za wanawake,nilikuwa na binamu yang walimsaidia xn ,and nw she iz very happy women do that my dia my b u can check me to take u thare
 

nashukuru kwa ushauri, tulichofikiria ni kumpa mtaji na kumfungulia account yake ya benki. unajua imefika hatua wanaishi kulea watoto mambo mengi hawashirikiani. lakini ndio hivyo jamaa wanaona kumkomoa ni kumuweka awe anakaa nyumbani.

ila hapo mwisho umenitisha aisee!!! kumbe mnatuviziaga tuu!!
 

Yaani ukipiga mpira tu nje ya uwanja, tunakupa red card...
 
Yaani ukipiga mpira tu nje ya uwanja, tunakupa red card...

kwa situation kama hiyo ya mpwa wangu ungekuwa ulishasepa saa mingi inaonesha!! wakati mwingine hata enemies huwa wanavumiliana.
 
kwa situation kama hiyo ya mpwa wangu ungekuwa ulishasepa saa mingi inaonesha!! wakati mwingine hata enemies huwa wanavumiliana.

hahahahaaaaaaa huyo ningemwendea kwa jet lee nikajifunze tai chi... nikirudi hadi dekio atashika.. hahahaaaaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…