Msaada wa Kisheria: Kwa Tukio Hili Mwajiri Anapaswa Kulipa Fidia Gani kwa Mjane?

Msaada wa Kisheria: Kwa Tukio Hili Mwajiri Anapaswa Kulipa Fidia Gani kwa Mjane?

Kingcobra

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
1,000
Reaction score
310
Wataalam wa sheria,

Salaam kwenu na poleni na majukumu ya kila siku.

Kuna Dada yangu mmoja mume wake alifariki akiwa njiani kutoka kazini kuerejea nyumbani. Ilikuwa ni mida ya jioni alipokutana uso kwa uso na lori yeye akiwa anaendesha pikipiki. Waligongana kwa kosa la mwenye lori na akafariki hapo hapo. Nimesema kwa kosa la dereva wa lori kwa sababu ndiyo rule ya mahakama na dereva wa lori alikiri hivyo.

Baada ya msiba, mwajiri wa mume wa dada yangu aligharamia sanda, jeneza, shada la maua na usafiri wa magari mawili kwa ajili ya kusafirisha kwenda kwenye mazishi ndugu wa marehemu pamoja na mjane. Pia, mwajiri alitoa rambirambi kama taasisi na michango kutoka kwa wafanyakazi na kutoka kwa makampuni yenye mahusiano na taasisi aliyokuwa anafanyia mume wa dada yangu.

Sasa nachotaka kujua ni je, sheria inasemaje kuhusu fidia ya mwajiri kwa mjane maana marehemu shemeji yangu ameacha familia ikiwa na watoto wanaohitaji matunzo na kusoneshwa. Je, alichotoa mwajiri kinatosha au kuna kingine zaidi ikizingatiwa kuwa marehemu alipata ajali akiwa ametoka kazini kuelekea nyumbani?

Tafadhali wajuzi wa sheria wanisaidie katika hilo ili nami nione ni namna gani tunaweza kumbana mwajiri.
 
Kwa kuwa hakuwa kazinina hakuwa anafanya kazi wakati ajali imetokea sidhani kama kuna la ziada. Ni vizuri kuwa amejitolea at least hayo.
 
Nafikili kwa hapo ungefikilia kudai bima au mmiliki wa gari aliyesababisha ajali.Kama una nia hii ya kudai bima tafadhali wasiliana na mimi. Mimi nahusika sana na Claim Settling agency.
 
kwakuwa mumewake hakuwa kazini hapo hakutakuwa na fidia yoyote kutoka kwa kampuni aliyokuwa anafanyia kazi
 
Vipi mmefika ofisi za Bima hapo mkoani kwake aliko mjane ambako ilitokea ajari? Na huyo mwenye loli la mchanga lililosababisha ajari mmewasiliana?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kwa kuwa hakuwa kazinina hakuwa anafanya kazi wakati ajali imetokea sidhani kama kuna la ziada. Ni vizuri kuwa amejitolea at least hayo.

thats not legal reasoning in employment law! kifupi ni kwamba mtu akiwa njiani kuelekea kazini yuko in the course of employment na akiwa njian kuelekea home akitokea kazini yuko in course of employment mpaka anapofika nyumbani kwake.
 
Katika hili hakuna suala la fidia unless kama unaweza ku argue kuwa mwajiri ni chanzo cha ajali hiyo au ametengeneza mazingira ya ajali hiyo au kuna namna angeweza kuizuia ajali hiyo lakini alishindwa kufanya hivyo.

Ili kutopoteza muda na resources kwa kufungua kesi ya madai dhidi ya mwajiri, ni vema kama nguvu zingeelekezwa zaidi kwa bima au/na pia mfuko wa hifadhi ya jamii (kama marehemu alikuwa mchangiaji) kama wanalo fao la kusaidia watoto/wategemezi.
 
Mfanyakazi akiumia wakati anaenda au kutoka kazini anstahili fidia, ili mradi mwajiri alikuwa akilipa hiyo workmen compensation, sina uhakika kuhusu akifariki. Kuhusu mafao kwa mjane na watoto, hapo mfuko husika wa hifadhi ya jamii unachukua nafasi yake baada ya wao kama ukoo kukaa na kuchagua msimamizi na wategemezi, kufungua jalada mahakamani na kuwakilisha madai kwenye Mfuko wa Pensheni husika.
 
kama mfanyakazi angekuwa njiani kwenda kufanya kazi za nje inamaana still yuko kazini na baada ya ajali walau ungekuwepo uwezekano wa kudai fidia kwa vile alikuwa anaenda kufanya kazi .. ila kwa kuwa alikuwa anaelekea nyumban sidhani kama kuna kitu kinachobana sana kwenye sheria kufidiwa .. ila cha msingi ni kuwasiliana na bina ya yule aliyesababisha ajali .. pia inatakiwa iwepo uthibitisho wa chanzo cha ajali
 
Katika hili hakuna suala la fidia unless kama unaweza ku argue kuwa mwajiri ni chanzo cha ajali hiyo au ametengeneza mazingira ya ajali hiyo au kuna namna angeweza kuizuia ajali hiyo lakini alishindwa kufanya hivyo.

Ili kutopoteza muda na resources kwa kufungua kesi ya madai dhidi ya mwajiri, ni vema kama nguvu zingeelekezwa zaidi kwa bima au/na pia mfuko wa hifadhi ya jamii (kama marehemu alikuwa mchangiaji) kama wanalo fao la kusaidia watoto/wategemezi.
Well said. I think this could be the best way to follow.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Back
Top Bottom