Msaada wa kisheria kwa wnafunzi hawa. WAMESHATESEKA VYA KUTOSHA

Msaada wa kisheria kwa wnafunzi hawa. WAMESHATESEKA VYA KUTOSHA

Joined
Jun 21, 2013
Posts
7
Reaction score
3
Kuna taasisi moja inayohusika na elimu ya juu hpa dar-es-salaam imewafukuza wanafunzi 45 kwa kosa la kufoji risiti za ada.Ni kweli makosa haya yalifanyika lakini taratibu za kumfukuza mwanafunzi hazikufuatwa kam student handbook inavyosema pamoja na university charter ya taasisi hiyo. Kabla ya ndugu hawa kufukuzwa waliambiwa walipe fedha hizo wataendelea na masomo lakini baada ya kufanya hivyo walifukuzwa moja kwa moja.
Kikubwa cha kushangaza ni kwamba walihojiwa na kamati isiyo halali tarehe 28 january baada ya hapo wakapewa barua za dismisal ambapo barua hiyo inasema kwamba maamuzi ya kuwafukuza chuo yalifanyika tarehe 8 january swali hapa ni kwamba kwa nini umhoji mtu wakati maamuzi yameshatendeka. Na inasemekana kwenye kitengo hiki imeshapita miaka mitatu toka wanafunzi waanze mchezo huu na mhasibu alikua hajaliona hilo hivi ukweli uko wp hpa? Baada ya kuja mhasibu mpya ndie aliyegundua huu mchezo na baada ya kugundua tu wakamtimua.
Kikubwa zaidi wanafunzi hawa wanapata mikopo kutoka students loans board na kwenye barua yao ya kufukuzwa waliambiwa taarifa zitatumwa loan board na tcu ili wasitishie huduma lakini uongozi wa taasisi hii haujafanya hivyo na kwa male wanaopata mikopo majina yao bado yanakuja chuoni hpo na ili uendelee kupata mkopo lazima bodi wapata matokeo yako ya kila semister na hawa jamaa hawajafanya mtihani wowote toka january but kule board kuna matokeo yao ambayo ni feki. Tunaomba msaada wenu wa kisheria kwani vijana hawa hawana pa kwenda na walijaribu kuonana na baadhi ya wanasheria but wakawa matapeli kwa kuwalia pesa zao na kazi hawajafanya na wanafunzi wapo mtaani wanateseka na hali ngumu ya maisha..........niliyoandika yote ushahidi upo wa maandishi...............TUNAOMBA MSAADA WANA JAMII
 
Simeon Manyaki vs Executive commettee & council of IFM [1984] HCD. Google usome hii kesi itakusaidia sana.
 
Huo ni wizi lazima wafukuzwe wewe ulitaka wazawadiwe au wewe ni mmoja wao? Nyambaf kabisa unataka kutetea wezi kwanza walitkiwa wachomwe
 
Sijawahi kusikia upumbavu kama huu. Wanafunzi wezi waliofoji risiti wasaidiwe kutetewa? What is going on with you Tanzanians? hawa wanatakiwa kufungwa jela, wezi wezi wezi, yaani tumefikia mahali wewe mtoa hoja huoni kwamba hawa vijana hawafaia kabisa hata kuitwa wanafunzi? hivi values zetu zimekwenda wapi?
 
Simeon Manyaki vs Executive commettee & council of IFM [1984] HCD. Google usome hii kesi itakusaidia sana.
hahahahaha daaaahhh na ile ya jamaaa wa engineering kule coet inaweza kuhusika..administrative law is in the air..!!!!!
 
Sijawahi kusikia upumbavu kama huu. Wanafunzi wezi waliofoji risiti wasaidiwe kutetewa? What is going on with you Tanzanians? hawa wanatakiwa kufungwa jela, wezi wezi wezi, yaani tumefikia mahali wewe mtoa hoja huoni kwamba hawa vijana hawafaia kabisa hata kuitwa wanafunzi? hivi values zetu zimekwenda wapi?

Huo ni wizi lazima wafukuzwe wewe ulitaka wazawadiwe au wewe ni mmoja wao? Nyambaf kabisa unataka kutetea wezi kwanza walitkiwa wachomwe
Kama mlikua hamjui ni hivi..kuna kitu kinaitwa right to be heard..!! kwenye principles za utawala..kimsingi utaratibu unatakiwa ufuatwe..wa kufukuza watu short of that reistatement inahusika..principle inakwenda hivi Ikiwa Mungu mwenyewe alimuita Adam kwenye bustani ya eden na kumuuliza yuko wapi hiyo ni baada ya adam kula tunda lisiloruhusiwa..je sembuse mwanadamu ndo awafukuze watu bila kuwahoji? inawezekana ni politics but thats how things are..
 
Msihukumu watu kufoji risiti, mi siafikiani na kitendo hicho ila pia huwezi jua sababu ya mtu kufikia hatua hiyo. Kuna watu mnakuwa kama vile hamjawahi kupata shida.
Kama kukosea wamekosa, basi na taratibu za kuwaadhibisha zifwatwe. Justice should be served accordingly not to leave loopholes for corruption.
 
You can not justify shida zako na wizi, wizi ni wizi tu, the fact kwamba nchi yetu inaongozwa na mijizi na mijambazi hai justify kuzalisha taifa la wizi, tunachotakiwa ni wote tuliona na right mind kupambana kurudisha value za watu wa kawaida kwa kupambana na hayo majambazi yaliyoshikilia nchi yetu kwa nguvu. Hakuna mjadala hapa wanafunzi wezi wa risiti wafukuzwe mara moja na kufunguliwa mashitaka, the right to be heard usiitumie kama kasuku ili mradi tu umejua neno lakiingereza bila kujua maana, waulize wanasheria wakueleze content ya kutumia right to be heard, right to be heard itawakuta mahakamani juu ya adhabu ya kupewa kama ni miaka kumi ama mitano toa upumbavu wako hapa. Mwanafunzi haibi, si risiti tu na hivyo kumaanisha wameiba hela, hata kuiba majibu ya mtihani ni kosa la kutosha kumfukuza na kumfungulia mashitaka, kizazi unachotaka kukitangaza wewe hakitakiwi duniani labda jehanam na sisi tunawatoto hatutaki waishie huko. shule imewashinda wakatafute shughuli nyingine si lazima kila mtanzania awe na elimu ya chuo kikuu unataka kuanzisha profession ya wizi? hovyo kabisa
 
Kama ushahidi upo ya kwamba walifoji risiti za benki, bora wapotezee kwani itibua sokomok lingine la benki kuwashitaki kwa kugushi nyaraka zake, kama hawakupewa muda mzuri wa kusikilizwa hilo nikokosa na kwasababu hiyo wanaweza kwenda mahakama kuu kuseek judicial review by filing an aplication in chamber summons, japo inaweza kutoa writ ya certiorari ila haitawafutia kosa la kugushi. Poleni sana
 
Back
Top Bottom