Msaada wa kisheria maswala ya bima

Wamalinyi

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2016
Posts
237
Reaction score
145
Habari,

Nilipata Ajali ya kugongana gari langu na lingine la kampuni fulani hapa jijini dar,Gari yangu ina third part ile gar iliyonigonga ina Comprehensive,Kesi ilienda nahakamani imeisha mwezi mmoja ulioisha yule dereva akatozwa faini elfu 40,000/=

Nikafuatilia nakala ya hukumu nikapata nikaenda polisi kuchukua final report na document zingine ili niende kwenye kampuni ya bima ya wale jamaa ili niweze kudai nitengenezewe gari yangu, sababu tokea mwezi wa nne gari yangu ipo gereji kusubiri bima wanitengenezee.

Nimepeleka vithibitisho vyote vya Ajali (documents zote pamoja na hati ya hukumu kutoka mahakamani) katika ile kampuni ya bima ili nilipwe, cha ajabu naambiwa mimi nimtafute alienisababishia ajali niende naye pale kwenye ofisi ya bima. Nikiwapigia simu walionisababishia ajali wananiambia Mwanasheria wao wa kampuni kawaambia kesi ilishaenda mahakamani dereva akalipa faini na kesi imeisha, kila gari itatengenezwa na bima yake.

Mimi bima yangu ni ndogo ya kwao ambao walinisababishia ajali ni kubwa.
Naombeni msaada wa kisheria.

Asanteni.
 
Ok. Kwanza kisheria wewe utalipwa na bima ya gari la dereva aliyehukumiwa..... Kwahiyo hapo katika maelezo yako document za police zitakusaidia kujua kampuni aliyokatia bima. Pili kampuni za bima siku zote huwa zinatafuta sababu za kwanini wasikulipe. Kwahyo hapo uwe unajua data zako vizuri na uwe na kila kinachohitajika... Tukija ktk msaada wa kisheria... Nskushauri nenda kwa kamishna wa Bima katoe maelezo yako utasaidiwa vizuri sana juu ya sheria za bima... Au kama vp mi nipo tayari kukusaidia mwanzo mwisho ila tutalipata baada ya kuwa tumekubaliana... Kama utakuwa bado haujafanikiwa ktk hayo... Asante

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
 
kama gharama ya kutengeneza iko chini ya milioni moja hawalipi ila juu ya hapo wanalipa hii ilinitokea mwaka jana niligongwa na daladala kariakoo ikabidi nibanane na dereva mpaka wakanitengenezea gari kwa kuwa gharama ilikuwa laki nane.
 
kama gharama ya kutengeneza iko chini ya milioni moja hawalipi ila juu ya hapo wanalipa hii ilinitokea mwaka jana niligongwa na daladala kariakoo ikabidi nibanane na dereva mpaka wakanitengenezea gari kwa kuwa gharama ilikuwa laki nane.
milioni4
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…