Msaada wa Kisheria,Nataka kuwasaidia wazazi wangu kupata fedha zao walizotozwa faini isivyo halali.

Super Sub Steve

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2011
Posts
17,404
Reaction score
10,900
Ni miaka mingi imepita kama sita hivi.Kwenye familia ya Baba yangu kulitokea ugomvi kidogo.Mdogo wa baba wa mwisho alienda kwenye shamba la kaka yake akachuma mazao yasiyofika hata thamani ya elfu ishirini.Sasa Yule kaka (Ndugu yao...Mimi namwita baba mdogo) akashtaki Kwa balozi na kesi ikafika hadi Kwa mtendaji wa Kijiji.Mtendaji wa Kijiji akasema ikasuluhishwe kindugu.Walivyorudi kusuluhisha kindungu kuna jirani moja ndio akawa kama msuluhishi.Na mdogo (Yule mdogo wao akina baba last born) akapatikana na hatia ya kumlipa ndugu yake.Yule ndugu yake (Kaka yake) akadai fidia ya Milioni mbili ,wakapunguziana ikalipwa milioni moja na Laki nane.Hiyo hela Kwa kiasi kikubwa ililipwa na.mzazi wangu maana wengine hawakuwa na uwezo akiwepo aliyefanya kosa.

Sasa kila nikitafakari Huwa naona kama ile faini haikuwa halali na huenda ilipangwa vile Kwa vile Mzee alikuwa na visenti hivyo walijua kuwa atamsaidia tu mdogo wake kulipa.

Je kesi kama hii inawezekana kufufuliwa na kuomba fedha zirejeshwe.Maana wazazi wetu walipotusimulia hii kesi sijawahi pata amani naona kama walionewa.
Naweza ifufua nikapeleka mahakamani ili kupata Haki?
 
Malizaneni kindugu tu mkuu kama mlivyomalizana mwanzo.

Hamna kesi hapo asee.
 
Asili ya kesi ni ubishi.... Sasa Hiyo kesi utakuwa unadai Wewe Kama Nani?
 
You have no locus standi pili you are time barred
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…