Msaada wa kisheria: ndugu zangu wawili, shule tofauti wamefutiwa matokeo na Necta

Msaada wa kisheria: ndugu zangu wawili, shule tofauti wamefutiwa matokeo na Necta

Zlatanmasoud

Member
Joined
Dec 19, 2010
Posts
71
Reaction score
16
Wadau naomba mwenye ushauri wa kisheria atusaidie, ndugu zangu wawili mmoja mwanamke na mmoja mwanamme, wanasoma shule tofauti wamefutiwa matokeo.
Hapa nyumbani ni majonzi matupu. Yaani bora wangeandilkiwa Div 0 kuliko hivi. Mwenye msaada nini cha kufanya atusaidie au kama imekula kwetu tujue pia. Ahsanteni.
 
kabla ya kusaidiwa taja sababu iliyopelekea kufutiwa matokeo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kwanza pole kwa hili. Nadhani unaweza kwenda baraza la mitihani na kufuatilia. Hila kwa matokeo ya mwaka huu kwa kweli usishangae ndugu zako kuwa na IV au 0, ila ni haki yenu kujua.
 
wameandikiwa W* yaani yamefutwa kwa tuhuma za udanganyifu

kama ameandikiwa W* co kwamba yamefutwa,yamezuiwa kwa muda 2 kutokana na sababu mbalimbali.so ni vzr ukawasliana na necta kwa maelezo zaidi.
 
Poleni Sana ila jitahidini muwasiliane na necta mapema iwezekanavyo.
 
wameandikiwa W* yaani yamefutwa kwa tuhuma za udanganyifu

Sio udanganyifu tu, pia kuna walioandika matusi, mistari ya bongo fleva na kuchora katuni kwenye answer book. Sasa waulize kama mawakili wanavyoongeaga na wateja wao wakupe hali halisi wao ni nini kimewasibu kati ya hayo. Wakikupa ukweli ndio uamue kwenda kukata rufaa ama kuangalia utaratibu wa maisha mwingine tu. Usije kukurupuka kwenda kuwalaumu BMT halafu ukakuta BMT wana ushahidi wa kutosha.
 
au ndo wale walioandika hip hop,
nenda kule baraza ukafuatilie.
 
aisee fuatilia baraza la mtihani nadhani w means withheld na sio kufutiwa mtihani.....
 
Back
Top Bottom