Msaada wa kisheria: Nilipigwa na kuvutwa korodani zangu na Mapolisi

kb52

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
336
Reaction score
109
Nakumbuka ilikua 2008 july. Nilipomaliza masomo yangu ya chuo na kwenda nyumbani kusalimu wazazi. Nikiwa hapo nyumbani..Mama yangu na wanafamilia kwa ujumla walikua wakilalamika juu ya suala ya maji ya bomba...ambayo yalikua hawayapati licha ya kila mwezi kuyalipia bill. Na hata yalivyokua yakianza kutoka...watumishi wa idara ya maji wa wilaya walikua wakijakuyafunga na kutuahidi watayafungulia siku ya pili. Tatizo lilidumu kwa miezi karibu saba.

Basi,kuna siku maji yalianza kutoka na ghafla wale watumishi kama kawaida yao wakaja hapo nyumbani kwa lengo la kuyakata. Ndipo nikawauliza kwann walikua wakiyakata...wakajibu:wanakata ili yaende kwa presha kwa mheshimiwa diwani ambaye anaishi jirani na kwetu. Kwa kweli sikuwaelewa na kwa kuwa walijitambulisha kua wao ni vibarua...nikawaomba wampigie boss wao ili atupe jibu kamili why tunakatiwa maji na huku bill tunalipa kila mwezi.

Boss hakua mbali na hapo...alifika na alikua kalewa sana....akatuhoji kwa ukali...hawa ni akina nani wanaokataa kukata maji. Wanatusumbua na vibill vyao vya sh.7000 wakati wengine wanalipa sh.20000. Kisha akachukua spanner na kuyafunga kwa nguvu.

Kesho yake...akajakuyafungua..lakini akauliza madada zangu kama nilikuepo nyumbani. Wakamwambia nipo. Akaondoka.

Majira ya saa 5 akaja na mapolisi wawili...wakasukuma geti na kunikuta uwani nafua...yule mtumishi wa idara ya maji akawaambia wanikamate. Wale polisi wakanifuata wakaniambia natakiwa kituo cha polisi. Nikawauliza kwa kosa gani....wakasema nitajua hukohuko....then..kwakua nilikua nimevaa kibukta tu niliwaomba niingie ndani kubadili nguo....wakakataa...wakasema niende ivo ivo kifua wazi. Mara ghafla wakaanza kunipiga...wakanitoa nje ya geti...kulikua na wenzao wanapita. ...wakashuka kwenye gari wakaanza kunipiga na kuniweka kwenye teksi iliyokua imekodishwa na yule mtumishi wa idara ya maji.

Niliendeshwa huku nikizungushwa mikono nyuma..huku nikivutwa korodan zangu. Na mara baada ya kufika kituo cha polisi...niliingizwa kwenye chumba cha mateso na kupigwa mpaka kuzimia. Nilizinduka badae...mwili wote ukiwa na damu...nimejikojolea na kujinyea...nilikua nikitoka damu sehemu zote...sikuweza hata kunyanyua mikono yangu wala kusogeza miguu.

Nakumbuka nilipelekwa polisi majira ya saa 5 asubuhi...but..nilipata fahamu saa tatu usiku. Ambapo nililazimishwa kusign malezo ambayo si yangu. Ndugu walifika kunipa chakula but ilishindikana....polis waliwagomea.

Kesho yake hali ilikua mbaya sana...nikapelekwa hospital kwa baskeli na polisi ambaye mara baada ya matibabu aliondoka na dawa nilizopewa na dakiktari. Kisha nikapelekwa jela siku ya ijumaa saa 10 jion. Na nilikaa huko mpaka jumatatu ambapo nilipelekwa mahakamani kusomewa mashtaka yangu....

Mashtaka yalikua ivi;-
1.(a) Nimemzuia mtumishi wa idara ya maji kufanya kazi yake
(b) Nimempiga na kumjeruhi mtumishi huyo

2. (a) Nimewazuia polisi kufanya kazi yao
(b) Nimewapiga na kuwajeruhi polisi

Kumbe wakati napelekwa kituo cha polisi...Mama yangu alipigiwa simu aende nyumbani kuniangalia. Na alivyofika akamkuta yule mtumishi wa idara ya maji na kuanza kumhoji why alileta mapolisi nyumbani na wakati yeye wanafanya kazi sehemu moja?..kwann wasingeyamaliza huko ofisin kwao....ndipo Mama yangu akasukumwa mara tatu na kupata hitirafu katika uti wa mgongo....alifanyiwa operation ya mgongo na kuwekewa pingili za prastic na chuma mwaka juz. Kisha yule jamaa alivyoona mama yangu anashindwa kuamka chini. ..akakimbilia polisi kumshtaki. So it was like ...the same day nasomewa mashtaka yangu mahakamani na mama yangu alikua akisomewa pia...kwamba....kampiga na kumdhuru huyo mtumishi wa maji. ...na kumzuia kufanya kazi yake.

Kesi ziliendelea...wote mimi na mama yangu tupata dhamana. But kesi ya Mama haikuchukua muda ikafutwa kwasababu mshataka alikua hatokei mahakamani. Yangu iliendelea toka 2008 hadi July 2012. Ikaisha na nilishinda kesi.

Nilijaribu kuandika barua kuanzia ngazi za chini kabisa hadi makao makuu ya polisi kitengo cha malalamiko bila mafanikio..

Niliandika pia kwa tume ya haki za binadamu b
 
Pole sana, nenda kituo cha sheria tafuta mtu wa sheria watakusaidia then uende pia Polisi Makao makuu kuna kitengo cha Makosa dhidi ya Binadamu omba kuonana na mkuu wa kitengo then umpe full story atakusaidia, kuna fidia lazima utapata. chuo uliendelea?
 
wakati mwingine nawaza binadamu anapataje kuwa na roho mbaya kiasi cha kumtesa binadamu mwingine namna hii. pole sana Mungu anakuona na atakutendea haki hata kama sio leo atalipizwa tu huyo aliyetumia cheo chake kukunyanyasa
 
Pole sana kaka, what goes around comes around na malipizi ni hapahapa dunian i can assure u it is just a matter of time.
 
Mzee tuko pamoja, nimenunaje? please update whatever is happening kuhusiana na hili!
 
Daaah aiseee!

Pole sana mkuu, kama uko Dar nenda kitua cha haki za bianadamu na msaada wa kisheria kipo pale kijitonyama karibu na Ustawi wa jamii waone Helen Kijo Bisimba na mama Lucy Nkya watakusaidia kwa asilimia mia moja mkuu!
 
Siwezi kuwapenda na sitakuja kuwapenda polsi wa nchi hii hata sku moja... So sad..
 
Kweliwe mvumilivu, mimi ningeshamalizana na huyo kibarua wa idara ya maji na askari wote walioshiriki, NINGESHAMALIZANA NAO KITAMBO!
 
Maelezo yako ni mazuri lakini ingekua vizuri zaidi kama ungetaja majina halisi ya wahusika na ni mkoa/wilaya/kata/kijiji/mtaa gani.

Yawezekana wahusika wengine.wameisha hamishwa kituo cha kazi ama wamestaafu lakini kukawa kuna wana/mwana JF anawafahamu akasaidia sheria kuchukua mkondo wake. Kama kuna aliye kwisha tangulia mbele ya haki tutacharaza bakora kaburi lake.
 
So sad,mwisho wa unyanyasaji huu umefika na tutakuwa katika mikono salama soon.
 
Pole sana nchi yetu ingekuwa na utawala wa kisheria ningeweza jabu kukushauri kilaywoman very unfortunately hatuna nakushauri tu peleka mahaka kuu kuliko zote chini ya jua
 
Im sharing this page wit my man, his excellency Peter Kibatala.
he MUST knw what to do. believe you me!
Pole sana!
 
Last edited by a moderator:
Kwani huyo ofisa wa maji alihamishwa,au aliwekea bodyguard?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…