Kalunguine
JF-Expert Member
- Jul 27, 2010
- 2,543
- 134
Mimi ni mtanzania mjasiriamali,katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita nilikuwa na kiasi cha pesa za kutosha katika akaunt yangu ya M-PAWA,nilipokuwa nikijaribu kutoa pesa kutoka mpawa kuja mpesa nikawa napata ujumbe wa kuwa sijafaulu kutoa pesa nilizokuwa nataka kutoa.
katika kipindi chote hicho nimekuwa nikipiga simu huduma kwa wateja mara kwa mara kuomba utatuzi wa shida yangu bila mafanikio.
jambo hili kwa kiasi fulani limenirudish NYUMA kiuchumi kwani pesa hizo zilikuwa ni za kununulia bidhaa ambazo kwa namna moja ama nyingine zingekuwa zimeniingizia faida ya takriban ya shilingi milioni 4.5 kwa kipindi chote hiki ambacho pesa zangu zimezuiwa kutoka katika line yangu.
jambo baya zaidi na la kushtua katika kipindi cha wiki moja nyuma kutoka sasa kila napoangalia salio langu la mpawa naambiwa salio langu ni tsh 0!
OMBI LANGU: sheria zinasemaje kwa mambo kama haya?
sheria mpya ya makosa ya mtandao inanilindaje ili nipate haki yangu?
#Vodacom