Sasa ni miaka 62 tangu MORTGAGOR a- mortgage eneo lake la ardhi kwa mtu (mortgagee) kwa kiasi pesa ambaye ana miaka 44 amekufa . Mortgagor amekufa some 27 years back . Watoto wa Mortgagor leo 2023 wanadai eneo hilo. Watoto wote wako above 45 yrs.....
Sheria inasemaje. je wanaweza kulikomboa? (redeem)
Kuna msemo wa kisheria unaosema "once a mortgage always a mortgage" ukimaanisha dhamana ya mkopo nidhamana tuu sio kitu ambacho kimeenda Moja kwa moja. Hivyo basi kinapaswa kurudishwa kwa mkopaji ikiwa atalipa mkopowake.
katika mazingira hayo kiukweli nimuda mrefu umepita. Sijui nikwanini msimamizi wa mirathi (ikiwa aliteuliwa) alishindwa kulimaliza Hilo kama sehemu ya wazi/kazi yake.
Lakini Hilo haliondoi Hali ya mmiliki wa ardhi husika au warithi wake kurejesha eneo.
Chamsingi nikuangalia kwanza msingi wa mkataba husika wa MORTGAGE yenyewe unamasharti Gani kuhusu mortgagee kushikilia hio mortgage kwa muda Gani. Wao walikubalianaje?
Pili kuangalia ikiwa mortgage ilisajiliwa kisheria. Lakini kwa muda uliopita si dhani.
Hili litawapa mwanga wakujua wapi muanzie ili kukutana na mortgagee na kuweza kulipa deni ili mrejeshewe ardhi yenu.
NB: Kumbuka mwenye mamlaka ya kufanya hayo kwa niaba ya marehemu ni msimamizi wa mirathi.
Kwahio ikiwa mnataka kufanya hili pendekezeni mtu atakaye ithinishwa na mahaka ili kuja kusimamia huo mchakato akiwa kama msimamizi wa mirathi.
NB: MORTGAGE IS REDEEMABLE, BUT IF MORTGAGOR PAYS ALL LOAN AS PER MORTGAGE AGREEMENT(CONTRACT)