msaada wa kisheria please,

msaada wa kisheria please,

mkatangara

Member
Joined
Feb 28, 2012
Posts
37
Reaction score
5
Mimi nina mtu nimempangisha nyumba yangu. mkoa tofauti ninapoishi,
Mkataba nimeuatach na email hii,
Kabla ya mkataba huu kwisha nilimtaarifu kwa njia ya simu mpangaji wangu kwamba nitapangisha kodi ya nyumba.
itakuwa 400,000 kwa mwezi.
Mpangaji wangu akiniambia tutaongea, cha kushangaza kabla hatujaongea huyo mpangaji amedeposit fedha kwenye akaunti yangu (kodi ya zamani), akanitaarifu, nikamwambia mbona hajatoa kodi niliyomwambia, akanijibu hawezi kutoa kiasi nilichomwambia ni kikubwa sana,na kuna nymba nyingi zenye bei ya chini kuliko yangu na nzuri kulipo yangu.
Hadi sasa tupo kwenye mgogoro mimi na yeye, mkataba wake umeisha zaidi ya week sasa,
ananiambia nimpe notice,(notice ya nini wakati nilishamwambia kodi itaongezeka?) kuna sheria yeyote inayohusiana na ishu kama hii?
nimemjibu simpi notice, kwenye mkataba tuliosaini hakuna notisi ya namna hiyo.
Nimemuambia ahame haraka aniachie nyumba yangu kama hana kodi ninayotaka mimi.
Nyumba yangu hiyo ipo Dodoma mjini ina vyumba 4. (kimoja masters),public toilet and public bath both independent, stoor, jiko, sebule na dinning, ipo ndani ya fense.
Nimempandishia kodi sasa nataka anilipe laki 4 kwa mwezi.
Anavyonizingua na mpango wa kuomba ruhusa ofisini niende nikamtoe kwa nguvu.
Utaratibu unakuwaje?
 

Attachments

mimi sio mzuri sana kwenye mambo ya sheria ila kwa sisi wapangaji wazoefu,kama mwenye nyumba hataki kuendelea na mkataba anatakiwa akupe notice ya mwezi mmoja kabla ya mkataba kwa maandishi.
nakusihi utumie hekima kumtoa huyo mpangaji maana ukitumia nguvu bila kufuata sheria anaweza kukubambika kesi ya kumvunjia himaya yake bila kibali cha kisheria
kwa ufafanuzi zaidi watakuja wanaJF wanasheria naamini wapo maana tumekuwa tukisaidiana sana haya mambo kupiti hili jukwaa
 
Back
Top Bottom