Msaada wa Kisheria plz, nimepata mimba na mpenzi wangu amenikataa

Msaada wa Kisheria plz, nimepata mimba na mpenzi wangu amenikataa

SENGATI

Senior Member
Joined
Jan 18, 2013
Posts
127
Reaction score
26
Hello JF! mm ni mwanafunzi wa chuo, nilikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mwanaume flan but kwa bahati mbaya tuliachana yapata mwezi sasa, nimepata mimba ambayo sikuitarajia na nilipomwambia mpenzi wangu ameikataa kwa madai eti hayuko tayari kubeba majukumu ya kulea. naomba msaada wenu kisheria nifanyeje?
 
mi si mwanasheria, lakini nionavyo mimi, kwa sababu hamjaoana na hujabakwa huo ni mzigo wako.
 
Tulia uzae umlee mwanao dada, utapoteza mda na raslimali fedha za kumlelea mwanao tu!
 
Hello JF! mm ni mwanafunzi wa chuo, nilikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mwanaume flan but kwa bahati mbaya tuliachana yapata mwezi sasa, nimepata mimba ambayo sikuitarajia na nilipomwambia mpenzi wangu ameikataa kwa madai eti hayuko tayari kubeba majukumu ya kulea. naomba msaada wenu kisheria nifanyeje?

Japo mimi si mwanasheria ila naamini huna cha kufanya zaidi ya kusubiri mtoto azaliwe nawe udai matunzo ya mtoto kama utaweza kuthibitisha kuwa jamaa ni baba wa mtoto.
 
Njoo tuilee..

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
kwanza sababu ya kuachana ni nini kama ni uaminifu dada huo cross wako cha kusubiri ni mtoto tena afanane na huyo jamaa ila sikushauri utoe binafsi nimeona wadada wawili mametoa wakiwa sec mpaka leo wanahangaika hadi wamekata tamaa hawashiki tena mimba
 
mpenzi wangu alikuwa mbishi sana, hakubali kushauriwa haf huwa hanishirikishi mambo yake na nikimuuliza ananijibu vibaya.. nimejisikia vibaya sana kuwa na hii mimba na ninaamini ni yakwake na amenichunia kabisa txt zangu hajibu, calls hapokei, last time alinitext kuwa anafight kutafuta kazi na hana pesa yoyote ya kunisaidia, nakaribia mitihan na hata cjui huko home nitasemaje coz ninaishi na mama tu ndo anayensomesha na kila kitu
 
Sasa mi kutoa sikushauri kabisa na ukijifungua kama uwezo wa home ni mdogo ni shuhuli kweli embu jaribu kumtafuta uongee naye mara nyingi kama mwanamke siyo mke wako huwezi kubali kirahisi sana ongea naye kama anakupenda atakubali tu wala usihofu hamna mtu asiyependa mwana
 
dada achana na uyo mweu ww lea haku utakalo shindwa bhana achana na sheria atajirudi tuuuu
 
ndg,nimesoma miaka mitatu chuo..tulikuwa na watu kama ao..nawalifanikiwa kwa ukubwa tuuu,akuna linalo shindikana jaman...shida atujiamini
 
Kwanza hii id ni ya jan 18 2013 post ya kwanza ulisema una demu anasema ana mimba yako ukaomba ushauri leo unasema una mimba wewe tena how this comes?
hawa wageni ni kiboko kwa kutunga singo zinazohit kitaa cha JF..labuda hiyo mimba iliingia kupitia mtandao pendwa a.k.a kameruni maana hilo nalo linawezekana!
 
mpenzi wangu alikuwa mbishi sana, hakubali kushauriwa haf huwa hanishirikishi mambo yake na nikimuuliza ananijibu vibaya.. nimejisikia vibaya sana kuwa na hii mimba na ninaamini ni yakwake na amenichunia kabisa txt zangu hajibu, calls hapokei, last time alinitext kuwa anafight kutafuta kazi na hana pesa yoyote ya kunisaidia, nakaribia mitihan na hata cjui huko home nitasemaje coz ninaishi na mama tu ndo anayensomesha na kila kitu

UNAAMINI NI YA KWAKE AU UNA HAKIKA?..Afu inaonekana umetembea na zaidi ya huyo coz you are not sure but you beliave ndo mimba yake.
Wewe hutumiagi condom eti eeh.
 
Polee mwaya..... Nenda mahakama ya watoto iko ndani ya mahakama ya kisutu, utaelekezwa cha kufanya. Lakini kwa sasa, kwa kuwa huyo mtoto hajazalia, hakuna sheria ya kukulinda. Ila mtoto atakapozaliwa unaweza ukafungua ombi hapo mahakama ya watoto kuomba matunzo ya mtoto kutoka wa huyo baba wa mtoto.. Nashauri uenda kwanza kwenye vituo vya kutoa msaada wa sheria kama wlac ipo kinondoni au tawla ipo ilala. I hope this helps... Goodluck
 
Back
Top Bottom