Msaada wa kisheria Sumbawanga kesi 125 zilibainika na kushughulikiwa

Msaada wa kisheria Sumbawanga kesi 125 zilibainika na kushughulikiwa

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Jumla ya Kata 10, Mitaa 15, Vijiji15, kesi 125 zilibainika na kushughulikiwa huku wananchi 25,780 walifikiwa ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga katika zoezi la msaada wa kisheria ambalo kilele chake ni leo Machi 6 Katika Mkoa wa Rukwa.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Nasri Saidi Kilusha wakati akizungumza na waandishi wa habari hii leo akielezea namna kampeni hiyo ilivyofanya kazi.

Amesema kampeni hiyo ya msaada wa kisheria imesaidia kuleta utatuzi wa migogoro mbalimbali ya wananchi katika Manispaa ya Sumbawanga, Huku akibainisha migogoro iliyochukua nafasi kubwa ikiwa ni pamoja na migogoro ya ardhi,mirathi ndoa na ile ya unyanyasaji pamoja na ukatili wa kijinsia.

 
Hizo Kesi 125 zimetatuliwa na zikaisha, au zilifikishwa tu kwa wataalam?
 
Back
Top Bottom