Msaada wa kisheria tafadhali

kapiki

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2011
Posts
382
Reaction score
104
Nimepigiwa simu na shemeji yangu kuwa leo 25.1. 2013 amekamatwa na askari wa kituo kidogo cha police Ijumbi wilayani Muleba. Hazari nilizoletewa na ndugu yangu aliye hapo ni kwamba mtuhumiwa amepelekwa katika Mahakama ya mwanzo ya Kashasha wilayani Muleba.
Wasiwasi wangu ni kuwa leo ni J1 na inaonekana kuwa kuna njama imesukwa kati ya police mlalamikaji na hakimu ili kumgandamiza mlalamikiwa. Mlalamikiwa anadaiwa kumtishia mlalamikaji kuwa atamuua. Ukweli ni kuwa huyu shemeji yangu alikuwa ni shahidi tu katika mgawanyo wa shamba la urithi ambapo mlalamikaji anaona huyu ndiye aliyetoa ushahidi uliomfanya akose shamba
 
Huko kwenye mahakama za mwanzo huwa kuna uonevu wa hali ya juu sana. Sitashangaa kabisa kama kuna njama imesukwa kati ya mlalamikaji, polisi, na hakimu maana hila kama hizo ni kawaida sana kwenye hizo mahakama (na hata za wilayani pia).

Mlalamikaji katishiwaje? Kwa mdomo? Kama katishiwa kwa mdomo, je, kuna shahidi au mashahidi? Kama kuna mashahidi, je, ushuhuda wao unafanana?
 
NANI ALIONEWA TUPE MFANO,wakati inapangwa njama ulikuwepo? hiyo kawaida ikoje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…