Kama kampuni imekumbwa na mdororo wa kiuchumi na imethibitika hivyo, kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004, kifungu cha 44, Mwajiri atapaswa kumlipa Mfanyakazi stahiki zifuatazo.
1. Ujira wowote wa siku alizofanya kazi kabla hajaachishwa kazi.
2. Malipo yoyote ya likizo ya mwaka na kama kuna malimbikizo ya likizo ambazo hakwenda.
3. Malipo ya notisi, ambayo ni mshahara wa mwezi mmoja.
4. Malipo ya kiinua mgongo, ambayo kiwango cha chini kabisa ni malipo ya mshahara wa siku 7, zidisha miaka uliyofanya kazi isiyozidi 10
5. Posho ya usafiri wako wewe mwenyewe na familia yako, pamoja na nauli ya mizigo, hadi mahali alipokuajiri Mwajiri wako.