Msaada wa kisheria tafadhali

Msaada wa kisheria tafadhali

nkolaniwe

Member
Joined
Jan 18, 2015
Posts
24
Reaction score
1
Mimi ni mfanyakazi wa kampuni moja ya ulinzi.

Miezi michache iliyopita client wa kampuni tunayoliilinda alidai kuibiwa mali yake baada ya uchunguzi wa kina upande wa kampuni yetu ya ulinzi walikana sisi kuhusika na tuhuma hizo na kuamua kutuhamishia vituo vingine vya kazi ila client yule aliyedai kuibiwa atutafuta tulipoamishiwa na kutufungulia kesi.

Swali langu la msingi kuna sheria inayoruhusu mfanyakazi kuendelea na kazi pindi ana kesi ya kujibu mahakamani? pili wa kushtakiwa ilipaswa iwe kampuni yetu ya ulinzi au sisi waajiriwa?

Tafadhali msaada wenu.
 
jamani wanasheria nisaidieni tafadhali.
Kuhusu kuendelea na kazi ni juu ya mwajiri wako ambaye anaweza kukusimamisha kazi ama kukuacha uendelee na kazi. Ila katika yote hayo ni kwamba utaendelea kupata mshahara wako wote; uwe umesimamishwa ama unaendelea na kazi.

kuhusu kushitakiwa ni kwamba unaweza kushitakiwa wewe pamoja na kampuni yako kwa pamoja
 
Kuna kitu kinaitwa vicarious liability ... Kwa facts ulizotoa ni wazi kosa lilitokea ikiwa ukifanya kazi za kampuni hivyo basi kampuni ilibidi ishtakiwe ndo labda ingekuwajibisha wewe..

Technically wanaotakiwa kushtakiwa ni kampuni maana huyo jamaa kwanza hakuingia mkatab na wewe bali na kampuni
 
Ndugu, kuna mambo mawili hujafafanua. Umeshtakiwa kesi ya jinai au madai?Kama umeshtakiwa kwa kesi ya jinai kuwa unahusika na huo wizi, basi kisheria unapaswa kushtakiwa wewe na siyo kampuni na kama umeshtakiwa kwa kesi ya madai kwa maana ulipe fidia ya vitu vilivyopotea basi kwa kanuni ya " vicarious liability" unapaswa kushtakiwa wewe na kampuni yako.
 
wakuu nimewaelewa hasa ndugu el nino lkn swali langu lipo hapa kampuni yangu bado inanitumia kama mfanyakazi je mm ninayo haki kuomba barua ya kusimamishwa kazi?
 
ndugu ayayoru mm nimeshtakiwa kwa kosa la jinai ictoshe tupo zaidi ya walinzi 15 katika shifti iliyotokea tukio na waliofunguliwa kesi hiyo n watano mmoja kati alipelekwa kimakosa kwani hakuwa karibu na eneo linalosadikika mali imebwa na kuhusu hili je?
 
Ndugu, kuna mambo mawili hujafafanua. Umeshtakiwa kesi ya jinai au madai?Kama umeshtakiwa kwa kesi ya jinai kuwa unahusika na huo wizi, basi kisheria unapaswa kushtakiwa wewe na siyo kampuni na kama umeshtakiwa kwa kesi ya madai kwa maana ulipe fidia ya vitu vilivyopotea basi kwa kanuni ya " vicarious liability" unapaswa kushtakiwa wewe na kampuni yako.

kwa mtazamo wangu kama bushi loya, ilivyo andikwa hapo juu ni sawa, ila ujue ukichukua dhamana ya kulinda ni lazima ujue ni nini unalinda kwenye eneo la mteja (kwa maandishi).

Mfano: ni vigumu kuwajibika kwa kuibiwa Kompiuta mpakato ndani ya ofisi wakati mlango hauja vunjwa na vingine kama hivyo....labla kama kuna mpango mahususi wa upekuzi kila mtu akitoka ndani ya ofisi.

Ila ukiachiwa magari..ukakuta limeibiwa saidi mira au spea tairi hiyo inakuhusu
Kwa tahadhari: nivizuri kukagua vizuri unacho kabidhiwa kulinda na kama kuna mapungufu ya wazi yawe kwa maandishi. Hii ni muhimu zaidi kwa mteja mpya ambaye huja jua tabia yake (ya kusingizia?)
 
Back
Top Bottom