...well, (samahani nitaendelea kukuuliza zaidi) ila position ya sheria ipo hivi, kuna namna mbili za ndoa, kwanza ile iliyofungwa aidha kidini, bomani au kimila, pili kama umeishi na huyo mwanamke kuanzia miaka miwili basi mnakuwa na hadhi ya kuwa mume na mke (presumption of marriage),
..hapo ndipo ambapo mmoja wenu anaweza kudai mali mlizochuma wote (division of matrimonial properties).
...kitu kingine, ni kuvunja ahadi ya kuowa (breach of promise to marry) mwenza (spouse) anaweza kudai fidia (i.e. compensation)
...
#naomba ufahamu kuwa sijatoka nje ya swali lako, nimeweka hivyo makusudi ili ufahamu ni wakati gani mwenza anaweza kudai)
....lakini kwa suala lako, i.e. kujipatia hela kwa njia za udanganyifu wala haliangukii kwenye mahusiano yenu, hiyo inawezwa fanya na mtu yoyote, kwahiyo huyo aliyekuwa mwenza wako anatakiwa athibitishe kuwa wewe ulijipatia hela kutoka kwake kwa njia za udanganyifu, pia anatakiwa aseme ni kiasi gani cha pesa, na ni vipi ulimdanganya.
....huyo hakimu anayekulazimisha umlipe atakuwa anakosea maana yeye anatakiwa asikilize kesi mpaka aridhike na ushahidi ndiyo atoe hukumu, maana hilo ni kosa la jinai na wala sio la madai ambapo labda lingehitaji usuluhishi (mediation).
...binafsi naona huo ni ukiukaji wa haki saili (Natural Justice) katika haki zako za kusikilizwa (right to be heard) na mwenendo mzima wa kesi na matakwa ya sheria.
....cha msingi, wewe shikilia kuwa hakuna pesa yoyote uliyopata kwa njia hizo mpaka hapo itakapothibitishwa, kama atatoa hukumu ikimpendelea mlalamikaji basi wewe utakuwa na haki ya kukata rufaa ndani ya siku 30. Cha msingi usikubali kulipa maana upande wa mashitaka ndiyo unajukumu la kuthibitisha hilo kosa (burden of proof) na siyo wewe.
...ukiona inakuwia vigumu, basi nitafute then nitakusaidia BURE kabisa, namaanisha hutolipa hata thumni kwangu.