Mpui Lyazumbi
JF-Expert Member
- Sep 1, 2010
- 1,901
- 410
Nianze kwa kuwaita akina Peter E. Mselewa na wazoefu woote wa mambo haya. Ni hivi ndugu yangu alimkopesha rafiki yake 3m na dhamana ilikuwa gari yenye thamani zaidi ya hiyo na ilipaswa kuwa refunded after one month bila riba yoyote. Waliandikiana kwa sharti kwamba isipolipwa fedha hiyo baada ya muda huo kupita mdai auze gari ili kurudisha pesa yake. Mmiliki alibaki na kadi na gari kwa kuaminiana. Sasa muda umeisha na inaonyesha jamaa kakopa tena pesa kidogo kwa utaratibu huohuo mahali pengine baada ya makubaliano hayo ya awali.Rafiki yangu anahaha namna ya kupata chake na kaja kwangu kuomba ushauri. Mimi nimewahi huku kupata inputs halafu nimshauri. Afanyeje jamaa yangu huyu?
Last edited by a moderator: