Mkuu naomba uisome post yangu ya mwisho na uielewe.Nimesema kuwa uwepo wa mwanandoa aliyeathilika na HIV na kama tatizo hilo halikujulikana kwa mwenza mwingine kabla ya ndoa na wawili hao hawajafanya tendo la ndoa.Mwanandoa aliyeathilika anaweza kuomba ndoa ivunjwe kwa kukosa tendo LA ndoa sababu ikiwa na HIV. Nano asiyejua HIV inapimwaje?
Tuache hayo mambo ya HIV.
Turudi kwenye ulichoandika kuhusu kuvunjwa kwa ndoa kwenye bandiko lako namba 2.
Uliandika hivi:
Isipokuwa taasisi ya ndoa inaweza kuvunjwa pale tu Mahakama itakapothibitisha kuwa ndoa hiyo imeharibika kiasi kwamba haiwezi kurekebishika tena(broken down irreparable).
Sawa.
Wanandoa husika wanaweza kuamua kuendelea kuishi pamoja au kuomba ndoa kuvunjwa kwa sababu ya kutokuwepo kwa tendo la ndoa baina yao.
Okay, hapa ni unamaanisha hata katika mazingira ambayo hayahusishi HIV, siyo?
Kukosekana kwa tendo LA ndoa au kushindwa kwa mwanandoa kutekeleza tendo LA ndoa baada ya kufunga ndoa kunampa nafasi yule aliyeshindwa kutekelezewa haki ya kuvunjwa kwa ndoa hiyo.
Kiini cha swali langu kipo hapo. Tukiweka pembeni suala la HIV, katika hali ya kawaida, endapo tendo la ndoa likakosekana kwenye ndoa, ukosefu wa tendo hilo unaweza ukawa ni msingi wa kuvunjwa kwa ndoa, si ndiyo?
Sasa basi, ili mahakama ifikie uamuzi wa kuivunja hiyo ndoa, kwa mujibu wa ulichokiandika wewe ni kwamba "taasisi ya ndoa inaweza kuvunjwa pale tu Mahakama
itakapothibitisha kuwa ndoa hiyo imeharibika kiasi kwamba haiwezi kurekebishika tena(broken down irreparable)."
Swali langu ni hili: mahakama huwa inathibitishaje kuwa tendo la ndoa kwenye ndoa ya fulani na fulani halipo? Je, mahakama hutegemea tu maneno ya muombaji/ mtaka talaka na maneno mtalaka mtarajiwa?
Kuna njia gani ingine ya kuthibitisha hali ya huo ukosefu wa hilo tendo?