Jamaa wawili wanapakana ambapo mmoja amejenga ukuta kuzunguka makazi yake,na jirani yake ndani ya eneo lake ameotesha migomba kabribu kabisa na mpaka.Mgomba mmojawapo umezaa tunda la ndizi ambayo imeninginia upande wa pili kwa jirani(yaani tunda lote la ndizi liko ndani ya ukuta wa jirani).Ni nani mmiliki wa tunda hilo?Je kuna kosa kisheria limetendeka?