Msaada wa kisheria/utaratibu

yahoocom

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2016
Posts
331
Reaction score
379
Habari ya jioni.

Kama kichwa cha mada kinavojieleza nnaomba niende moja kwa moja kwenye mada.
Nilikubaliana na rafiki yangu kuwa tushirikiane katika biashara ya uwakala. Yeye akaleta line ya till (sikununua) alafu mimi nikaingiza float na akapewa kijana ambaye usimamizi wa biashara kwa ujumla ulikua chini yangu. Baada ya kufanya biashara kama wiki tatu nikaona salio la commision na gharama haviendan yaan hasara nikaamua kusitisha biashara. Na nikafanya utaratibu wa kuirejesha.

Kuirejesha alimuagiza rafiki yake nikampatia na akamfikishia kesho yake akanitaarfu line mbovu. Nikamshauri kuipeleka ofis za tigo ili irekebishwe ila akanambia document zilotumika sio zake bali za kaka yake na huyo kaka yake tayar amemuuzia hiyo line huyu ambaye Mimi nilimkabidhi/aliyeagizwa kuja ichukua kwa Tsh200 000. Kaka yake alivoelezwa habari za line kutofanya kaz hakutaka elewa na akasema huyu mdogo wake afidie iyo laki mbili ili yeye abaki anashikana na mm kwamba nilipe 200000. Mimi nikamkatalia na nikamwambia iyo line ina commision yangu hivo cha kufanya ipelekwe ofisin ili irekebishwe ili na mm nipate iyo pesa. Nikapewa taarfa kuwa docs zilipotea. Nikamwambia Mimi siwezi lipa iyo lak2.

Sasa juz ijumaa akareport police nikaitwa jana jmos na nikaitikia wito. Case ikawa hiyo mimi nikamwambia afande kuwa hii sio case kwa sababu akipatikana mwenye line tunakwenda ofis za tigo line inarejeshwa. Tukavutana hapo ikaonekana mwenye haki ni aliyeriport case kwamba sasa kwa kuwa tumeshindwana niwekwe rumande kwa ajili ya kupelekwa mahakaman Jtatu kwa case ya uharibifu. Mie nikamkatalia kwanza sijaharibu kitu na huyu aliyeleta habari ya kuharibiwa line sio mwenye line, kwanza kuwa nayo tu ni makosa. Akatuambia tukae tuongee tena wenyewe. Mie nikamwambia tuwasiliane na mwenye line ndo atuambie lini aende ofis za tigo kurekebisha. Akasema yupo Tabora na ofisi za tigo zipo mbali hivyo hana nauli mie nikaona isiwecase nikamuuliza sh ngap akasema elfu 10 nikamtumia.

Tukarudi kwa afande tukampa makubaliano kuwa alhamis ataenda ofisin hivyo tutapata mrejesho na kupeleka kituon lakini suala lipo waz kuwa huyu afande anataka niilipe iyo pesa (na anaonekana kutokuwa na uelewa kabisa hata wa mambo madogo ya kisheria) na mm naona wala hakuna uhusiano wa mimi kulipa iyo lak2.
Wazo kubwa nililonalo ni kwenda TCRA kuriport ili izuie/iharamishe hii biashara ya kuuziana line ya simu kwani imeonekana huyu mwenye line hataki kutoa ushirikiano kwa kuwa hana cha kupoteza line ameshauza na pesa kapokea. Naombeni ushauri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole lakin ni somo kwamba usimuamini mtu katika biasharaa hata kama ni baba au mama yako, watu wengi walifeli hapo,
Alafu usifanye biashara kwa kuzoeana tu, kuweni n.a. maandishi, nakushauri uende mwenyewe tigo kuulizia watakupa ushauri zaidi
 
Pole lakin ni somo kwamba usimuamini mtu katika biasharaa hata kama ni baba au mama yako, watu wengi walifeli hapo,
Alafu usifanye biashara kwa kuzoeana tu, kuweni n.a. maandishi, nakushauri uende mwenyewe tigo kuulizia watakupa ushauri zaidi
Nimeshafika tigo, wapo straight wanataka washughulike na mteja wao ambaye ndiye mwenye line na sio mtu mwengine. Sio mimi wala huyu mdogo wake!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…