Naenda moja kwa moja kwenye mada, mama yangu ana tuhuma za udanganyifu wa mtihani huu wa primary, yeye anadai hakukuwa na kitu chochote alichofanya ndani ya chumba cha mtihani. Sasa tatizo mkuu wao amedai atawapeleka mahakani, je kwa hili adhabu gani inaweza kutolewa? je nikimtafutia mwanasheria ushindi wa kesi unawezekana? Naomba msaada wandugu maana ameshindwa hata kusheherekea chrismas vema. ASANTE
Katika historia ya baraza la mitihani tz sijawahi kusikia mtu kapelekwa mahakamani kwa kosa hilo. Huyo mkuu ana hila tu! Muambie mama amuambie ampeleke mahakamani tu watamalizana huko. Hukumu haitolewi siku moja, akitajiwa kesi hapo ndo ufikirie cha kufanya. Ma-bush lawyer tupo tutakushauri,lol! Muambie mama ale pilao, maisha yenyewe mafupi!
Unless ithibitike kuwa huo mwandiko uliofanana kwenye karatasi za majibu ni wa huyo mama yako, sidhani kama ana kosa lolote.ni mwalimu wa primary na ushahidi uliopo wameambiwa majibu ya watoto yamefanana isivyo kawaida