kwa ufahamu wangu kampuni ili ifikiye vigezo vya kuuzwa lazima kuwe na maamuzi ya body ya directors ambayo itahalalisha kuuzwa kwa kampuni husika,miongoni mwa mambo yanayotakiwa kuwekwa sawa ni kuangalia maslahi ya wafanyakazi na kampuni kwa ujumla ikiwamo na kulipa madeni ya kampuni kama yalikuwepo.Kama kuna wafanyakazi lazima kutakuwa na makubaliano kati ya mnunuzi na muuzaji iwapo atawachukua au waachishwe kazi,na iwapo makubaliano hayo yatakuwa yamefanyika kabla basi kutakuwa hakuna utata na waliokuwa hawana mikatabaa lazima hatima yao ijulikane kabla ya kuuzwa kwa kampuni,itakuwa ni hiari ya mnunuzi wa kampuni kuendelea na waliokuwa hawana mikataba kwa hiyari yake mwenyewe.