Msaada wa kisheria

french

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2017
Posts
3,572
Reaction score
3,726
Salaam,

Mimi nina kiwanja changu hapa Dar. Upande wa kushoto wa kiwanja changu nikaamua kuwacha njia ya watu kupita na magari madogo. Sasa mtu ninaepakana nae kaamua kupanda mahindi kwenye ile njia. Hivyo kufanya watu wasitumie ile njia na wakitaka kupita wanapita kwenye kiwanja changu. Juzi nimepeleka mchanga na kokoto kwenye site yangu, lori la mchanga likatumia ile njia yenye mahindi na kufweka mahindi yote. Sasa jamaa amenishtaki polisi akiomba alipwe. Hivi kesho naenda polisi. Hii imekaaje kisheria? kweli anastahili kulipwa huyu jamaa.
 
Viwanja vina mipaka kama hio njia ipo kwenye mpaka wako, au kama unayo ramani ya kiwanja basi nenda nayo polisi. Huo utakuwa ushahidi wako
 
Viwanja vina mipaka kama hio njia ipo kwenye mpaka wako, au kama unayo ramani ya kiwanja basi nenda nayo polisi. Huo utakuwa ushahidi wako
inaonekana ni vile viwanja ambavyo avina mipaka yakuleweka/avijapimwa na apo wataingia kwenye mgogoro mwingine wa mpaka.
 
inaonekana ni vile viwanja ambavyo avina mipaka yakuleweka/avijapimwa na apo wataingia kwenye mgogoro mwingine wa mpaka.
Yeah. Ni vile viwanja ambavyo havina mipaka. Lakini karatasi za jamaa aliyeuziwa hazionyeshi kama ameuziwa njia. Ameuziwa kiwanja tu, na mwenye kiwanja akaamua kutoa njia. Sasa huyu jamaa anadai njia ni ya kwake ameuziwa pia, kwa hiyo anapanda mazao kwenye hiyo njia
 
dah apo itabidi mpate mashahidi wengine wanaojua mipaka ya maeneo yenu bila hivyo kila mtu atakuwa anavutia kwake.
 
dah apo itabidi mpate mashahidi wengine wanaojua mipaka ya maeneo yenu bila hivyo kila mtu atakuwa anavutia kwake.
Aliyeniuzia kiwanja yupo na amekana mbele yangu na mbele ya huyo mwenzangu kama hajamuuzia njia. Ila jamaa anasema walikubaliana kwa mdomo kuuziwa njia. Yaani ndio nimejua wakuria watata sana.
 
Aliyeniuzia kiwanja yupo na amekana mbele yangu na mbele ya huyo mwenzangu kama hajamuuzia njia. Ila jamaa anasema walikubaliana kwa mdomo kuuziwa njia. Yaani ndio nimejua wakuria watata sana.
ataki kukubali alidanganywa na pia ukumuona alipoanza kulima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…