Msaada wa kisheria

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2007
Posts
4,120
Reaction score
3,468
Nina ndugu yangu alikuwa na kesi alishitakiwa kwa wizi wa matunda toka shambani. Aliyemshtaki ni mvamizi katika shamba hilo. Huyu ndugu yangu alikuwa anachunga matunda yake. Mvamizi huyu wa shamba ambaye anadai shamba na matunda ni vyake alienda mahakamani.

Kesi imeendeshwa na kumpa ushindi huyu ndugu yangu. Akaachiwa huru baada ya hakimu kusema ushahidi ni wa kujichanganya sana.

Mshitaki akakata rufaa. Akidai hajaridhika na uamuzi wa mahakama. Anasema mahakama haikuzingatia evidence alizozitoa hivyo anaiomba mahakama ya Wilaya ipitie upya mwenendo mzima wa kesi.

Swali langu:

Huyu ndugu yangu ambaye mahakama ilimuona hana hatia hii karatasi ya rufaa anatakiwa afanyiwe nini kisheria? Je kuna jambo anatakiwa kujiandaa siku ya kufika mahakamani?

Swali hili limekuja baada ya Hakimu kumwambia aandae majibu ya kumjibu mrufani. Je ni sahihi?

Kama hana imani na mahakama ya mwanzo mshitakiwa ajibu nini katika rufaa hii?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…