Naomba kujua yafuatayo sheria inasemaje.
Mfano mwanaume ameoa mke wa ndoa na hawana watoto kabisa na ikatokea yule mwanaume akafariki na wakati kabla hajafariki aliacha osia kuwa atakayeridhi mali zake zote ni mtu mwingine kabisa labda mtoto wa kaka yake. Sasa hapo sheria inasemaje kwa yule mke wa ndoa ataachwa bila kitu au anaweza kudai.naomba kujua kutoka kwa wanasheria.
mfano mimi mkristo inakuajae tafadhali
Kuwa makini kidogo, na maelezo yako. Unasema wosia au urithi? Yote si kweli, wosia hawezi kumpa mrithi mmojawapo autunze, sheria inakataza. Unapewa mtu ambaye sio mrithi autunze kama haukutunzwa benki, msikitini, kanisani etc. Na urithi hivyo hivyo hawezi kumnyima mrithi halali bila sababu ya msingi.sheria ya mirathi ya ipo wazi kidgo, inampa marehem maamuzi ya nani ampe wosia, halazimishwi wala hachaguliwi m2 wa kumpa wosia, kama aliamua wosia wake uende kwa m2 mwingine ni sawa, lakini mali hiyo katika wosia isiwe mali ya wanandoa, bali iwe ya marehem.
kama ni mali ya wanandoa, mke atatakiwa apate sehem yake kama sehem ya jasho lake.
kuna kesi ambazo zimeshawahi kuamriwa, kuwa marehem ana haki ya kumchagua m2 wa kumuandika kwenye wosio, akiwa katika utimamu wa akili.