Msaada wa kisheria

Kyawanjubu

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2017
Posts
2,452
Reaction score
2,197
Wakuu habari zenu.

Ndugu zangu me niko Arusha mitaa ya Njiro Nanenane hapa kwenye kijiwe changu ninapofanyia biasha ndo inafanyika mikutano ya kampen juzi alikuja Mrisho Gambo Kufanya kampeni.

Yalibandikwa mabango mengi kwenye flem za biashara, leo kuna dogo jirani yangu anafanya kazi ya kuchomea akabandua bango pale mlangoni kwenye ofisi yao. Kuna wamama wakamuona, wakaita wana CCM wakasema apelekwe Police me nikawa nawambia dogo akipelekwa police mnapata faida gani ?

Maana sisi ni majirani kuna maisha baada ya uchaguzi kweli wameita police wanasema me nimewatishia maisha difenda imefika imebidi nisepe yule dogo kabebwa, saiz napigiwa simu naambiwa kuna wanaccm wapo pale dukani kwangu wanataka kubeba vitu vyangu.
 
Kuna mambo mengine ya kijinga..kwa hiyo na wewe umejificha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…