MSAADA wa KISHERIA

MSAADA wa KISHERIA

Joined
Jan 30, 2013
Posts
71
Reaction score
9
Jamani nahitaji ushauri wa kitaalam,
Nimeolewa ni miaka mingi sasa, ila kwa bahati mbaya Mungu hajatujaalia kupata watoto wa ndoa. Lakini mume wangu yeye anadaiwa kuwa na mtoto kabla ya ndoa.
Ninashiriki sana kwa hali na mali katika kuleta maendeleo kifedha katika ndoa yetu, tuna biashara zilizo na mafanikio sana. Swali langu ni je inatokea mpaka nafikia umri wa kutoweza tena kuzaa, nini haki yangu pindi muda wa mirathi ukifikia? Maana sheria itamtambua mtoto wa mume wangu tu na wakati ki ukweli mimi ninamchango ktk mali hizi kwa asilimia 60%.
Nini nifanye ili nisije kusumbuana na wenye tamaa za mali. Ya Mungu mengi.
 
Kwa sababu wewe ni mke tayari hapo mirathi haina shida kabisa na si kweli kua sheria inamtambua huyo mtoto pekee, wewe kama mke una nafasi yako pia, lazima haki yako ipo tu ila ni vizuri kama wewe ma mumewe mkiona ni vema muandike wosia ili mmoja akitangulia mali zigawiwe vp(Sheria ya ndoa, Sura ya 29 kama ilivyorudia mwaka 2002).
 
naomba nielekezwe, kuna bwana mmoja aliwekwa ndani kwa tuhuma za mauaji lakini baada ya muda wa miezi saba ndani imebainika kuwa hana hatia, na yeye anataka kuanzisha kesi (kuishitaki jamhuri) ili apate fidia afanyeje?
 
Anzisha thread yako hapa umedandia treni ya mwingine, hutosaidika vizuri
naomba nielekezwe, kuna bwana mmoja aliwekwa ndani kwa tuhuma za mauaji lakini baada ya muda wa miezi saba ndani imebainika kuwa hana hatia, na yeye anataka kuanzisha kesi (kuishitaki jamhuri) ili apate fidia afanyeje?
 
haki unayo na kurithi utarithi ila kama alivyosema mheshimiwa hapo kama mnaelewana na mumeo vizurihana upendeleo kwa mwanake au mama ake huyo mtoto aandike wosia
 
Back
Top Bottom