lucasogutu
Member
- Nov 24, 2010
- 48
- 13
Naja kwenu kwa msaada wa kisheria.
Mie mwajiri alisitisha mkataba wangu kinyume na taratibu kwa sababu hakufuata taratibu wala sheria za kazi.
Baada ya kuona hivyo nilienda baraza la mapatano na usuluhishi wizara ya kazi (CMA) ambapo mwanasheria alitushauri tumalize shauri hilo kwa mapatano.
Tulikubaliana ya kuwa mwajiri anilipe mishara ya miezi sita.
Sasa siku ya kwenda kuchukua cheki nilishtuka kuona askari wakinivamia na kuniweka chini ya ulinzi wakidai kwamba wao ni wapelelezi na ninashitakiwa kwa kutishia kuua meneja wa kampuni niliyokuwa naifanyia kazi.
Kulitomea mabishano lakini niliwaomba wanisubiri nichukue malipo yangu kisha twende.
Niliingia ndani nikapewa barua iliyoelekeza kwamba nilipwe na baadae vocha nikaanza kusaini hati ile ya makubaliano.
Wakati nasaini ya mwisho wakanipa cheki kuangalia nikakuta cheki imeelekezwa kwangu lakini una muhuri wa Twiga benki account payee.
Kuwauliza wakajifanya hawajui na baadae wakasema nilikuwa nadaiwa benki.
Swali langu ni hivi katika shauri lilidumu zaidi ya siku 107 mwajiri hakusema nadaiwa. Hata kwenye hati ya maelekezo haikusema pesa hiyo iende Twiga.
Jitihada za kuwaomba warekebishe zimeshindikana naomba msaada kisheria ili nipate haki yangu.