Msaada wa kisheria

Msaada wa kisheria

Complicator EM

Senior Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
155
Reaction score
39
Kuna rafiki yangu alikuwa anafanya kazi kiwandani sasa ukatokea wizi fulani yeye na wenzake walipelekwa mahakamani na kusimamishwa kazi hapo hapo lkn waliendelea kulipwa mishahara.
Sasa kesi iliyoko mahakamani wameshinda na mahakama imesema hawana hatia je kwa wajuvi wa sheria nini kinafuata baada ya hapo ili warudi kazini?
 
Kuna rafiki yangu alikuwa anafanya kazi kiwandani sasa ukatokea wizi fulani yeye na wenzake walipelekwa mahakamani na kusimamishwa kazi hapo hapo lkn waliendelea kulipwa mishahara.
Sasa kesi iliyoko mahakamani wameshinda na mahakama imesema hawana hatia je kwa wajuvi wa sheria nini kinafuata baada ya hapo ili warudi kazini?

hIcho kiwanda ni cha serikali au???
 
Maelezo yake kama yalivyo:

Nilikuwa nafanya kazi kwenye shirika moja la umma hapa nchini.
Kulitokea tukio la wizi mm na wenzangu tukakamatwa na kupelekwa mahakamani, kesi ile imeunguruma na hatimaye tumeishinda jamhuri kwa mahakama kutuona hatuna hatia.
Kwa upande wa kazini tulikuwa tumesimamishwa kazi kwa tuhuma ya wizi lkn mshahara tulikuwa tunalipwa.
Sasa mkuu nisaidie baada ya kesi hii kwisha mahakamani nini kitafuata ili kurejea kazini?

Nikamwambia ngoja nikaulize jf!
 
Wanarudishwa kazini. Kama wana marupurupu ya likizo wanapewa. Mwendo mdundo. Waendelee kuvizia dili lingine ila wajue sasa wanaangaliwa kama na macho ya mamba
 
Iwapo kesi imekwisha na wameshinda wana haki zifuatazo;
  1. Kurudishwa kazini mara moja kunakofanyika kwa wao kurudi kwa muajiri wao na kuwasilisha barua yao iliyo ambatishwa na nakala za hukumu za kesi yao ikimjulisha kwamba kesi imekwisha na wao wameshinda nasasa wamerudi kazini
  2. Kumfungulia kesi ya madai Muajiri wao kudai fidia iwapo tuhuma zilizowakabili ziliwaathiri kwa namna yeyote
  3. Naiwapo muajiri atakataa kuwarudisha kazini basi hapo kuna wrongful termination na wanatakiwa kumfungua shauri CMA .ndani ya siku thelathini tangu wamjulishe muajiri niayao ya kurudi kazini nayeye kuwakatalia
 
Asante sana kwa maelekezo yako ya kiseheria, sasa inakuwaje pale mwajiri unapomweleza umeshinda kesi mahakamani hlf akadai eti bado kuna taratibu za kinidhamu inatakiwa zifuatwe ikiwemo kusikilizwa kwa shauri lako na vikao vya nidhamu tena.
 
Back
Top Bottom