Msaada wa kisheria

krenea

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2014
Posts
405
Reaction score
160
Ndugu zangu wanasheria nahitaji kufahamu taasisi ipi inaweza kunisaidia katika mchakato wa talaka uliopo mahakamani ili kupata haki na stahiki zangu na watoto bila kutozwa fedha?

shauri langu liko Dar es salaam.Asanteni.
 
Kiukweli sheria ni taaluma hivyo ni bora ukatafuta pesa ili upate huduma ya kisheria ipasavyo ila kama uchumi wako ni dhaifu ninakushauri uende kwenye vituo vinavyotoa msaada wa kisheria ila kumbuka tu hakuna kitu cha bure kabisa
 
Kajaribu kuomba pale kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) maeneo ya sayansi-kijitonyama, huwa wanawasaidia watu kupata haki zao pale wanapojieleza vizuri
 
Ndugu zangu wanasheria nahitaji kufahamu taasisi ipi inaweza kunisaidia katika mchakato wa talaka uliopo mahakamani ili kupata haki na stahiki zangu na watoto bila kutozwa fedha?

shauri langu liko Dar es salaam.Asanteni.

Kama upo Dar es Salaam, watafute NOLA (National Organization for Legal Aid), au nenda kwenye Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Ikithibitika huna uwezo wa kugharamia mchakato huo, utasaidiwa.
 
ipo taasisi inayotoa msaada wa kisheria tena bure kabisa, fika Temeke U/Taifa karibu na ofisi ya mkuu wa wilaya utakutana na wataalam watakao kusaidia
 
kwanza nenda mahakama ya mwanzo ukiwa na cheti cha ndoa na Sababu muhimu za kuvunja lipi pesa ya kufungua kesihaizidi elfu mbili pia omba mgawanyowa mali,matunzo ya watoto kwa kila mwezi na talaka na baada ya mahakamabkujiridhisha kuwapo na ndoa utaambiwa ombi lako limekubaliwa utakuwa mtu kuolewa tena ila kwa waisilamu baada ya kipindi cha EDA na utapewa talaka ndani ya siku arobaini baada ya kesi kuhamuliwa ikiwa na matunzo, na mgawanyo wa mali wasiliana nami 0757001400
 
sheria ya mirathi iliyotungwa na bunge la Tanzania inasemaje kuhusu nafasi na utekelezaji wa wosia ulioandilkwa na matehemu mwenye mali ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…