Msaada wa kitaalam na makadirio ya ujenzi wa nyumba

Msaada wa kitaalam na makadirio ya ujenzi wa nyumba

aminiusiamini

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2011
Posts
3,577
Reaction score
2,224
Wana Jamii,

Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa maono ya kutaka kujenga nyumba kwa ajili ya familia yangu. Nimekutana na threads mbili tatu kuhusu ujenzi, lakni nimeona sio haba kuomba ushauri kwa wale waliotangulia katika hili.

Kama mnavyojua, nchi yetu kila mtu anataka kupiga cha juu na hakuna uaminifu kabisa katika mambo mengi. Mimi nina mpango wa kujenga nyumba ya ghorofa ya vyumba vinne, kimoja chini na vitatu juu.

Mpango wa nyumba yangu kwenye ramani ni mzuri kwakweli, na nina hamu sana kuiona inakamillika. Ninachopenda kuuliza; je, kwa kuanza phase one tu kwanza, msingi mpaka kupaua nimeshatenga 20,000,000 tsh, kwa kuanza inatosha?

Kwa mjengo wangu najua itakula zaidi ya hiyo na sio shida kwa hilo, ila napenda kusikia mitazamo ya wengine wanaonaje. Na wale mafundi wasiobabaishaji wanalipwaje. Nitajibu maswali kama mwongozo wa kuweza kupata majibu sahihi kutoka kwenu.

Mafundi mwashi wanalipwaje na wapi naweza kupata matofali au nifyatue mwenyewe?

Kuhusu nyumba, ni vyumba vinne, vitatu juu na kimoja chini. Sebule mbili moja juu na nyingine chini, jiko na store/ laundry area na dining area.

Mawazo yoyote na hata maelekezo nitashukuru.
 
Mil 20???? Haitoshi ila ni nzuri kuanzia. Ila inategemea kiwanja chako kipo wapi. Kama ni kwenye slope utashangaa...inaweza kuishia kwenye jamvi.

Cha msingi ni control ya nondo na cement....maana cement inalika kweli kweli

Sehemu nyingine tamu ni slub....unaweza imba haleluuuuiiiyaaaaaa....

Ila anza ujenzi usiogope...mdogo mdogo utafika
 
Tahadhari na mafundi wa mtaani.
Ghorofa ni hatari usipoweka msingi imara na vipimo. Pia tofali kuwa mwanagalifu.
 
Kaka 20M kwa nyumba ambayo ni ghorofa ujenge mpaka upaue?? That is unrealistic....itakusogeza mahali fulani lakini sio mbali

Hiyo 20M nilitumia kujenga nyumba yangu moja ambayo ina 2 bedroom, Master bedroom 1, public toilets, jiko, sebule, mashimo yote mawili ya mfumo wa maji taka, kupaua na kuweka bomba za umeme tu na kuzichapia....20M ikaishia hapo na nikabaki na chenchi ya tofali kama 250chini na mchanga tripu 4 chini (kwa nilipojenga Moro trip moja ni 60,000)

Hivyo kwa structure ya ghorofa nina amini haitakufikisha mbali na kama mdau alivyosema, kama kiwanja kimekaa vibaya unaweza jikuta unaumia kwenye msingi wa jengo lako

Ila kama umedhamiria na umejipanga usiogope kujenga maana ujenzi wa wengi wetu ni wa "mdogo mdogo"...

Kuhusu mafundi mimi nilifanya hivi, kwa kuwa gharama za manunuzi ya vifaa vya ufundi ni juu yangu, nilichofanya nilikaa na fundi niliyeamua kumtumia tuka-negotiate gharama halisi ya ujenzi. Nikatengeneza ka mkataba ambako kalionesha nitamlipaje. Kwa kuwa makubaliano yetu ya awali ilikuwa ni ajenge mpaka boma likamilike (yaani tofali mbili za juu baada ya beam) nilikubaliana nae kuwa nitamlipa kwa awamu nne. Awamu ya kwanza ni advance kabla hajaanza kazi (hii hasa kwa kuwa nilitumia local fundi ila ukitumia kampuni - kitu ambacho najua inaweza kuwa ngumu kutokana na gharama zao - usilipe in advance) nilimpa 25%, akimaliza msingi na kumwaga jamvi nitampa 25% akipandisha kuta mpaka level ya mwisho ya madirisha kabla ya kumwaga beam nitamlipa 25% na inayobaki nitamlipa mara baada ya kumaliza kujengea zile tofali 2 za juu

Hii ilinisaidia sana maana hawa mafundi wetu wa mtaani bwana wanakuwa na mambo mengi sana na wakati mwingine hashindwi hata kukwambia niongezee kiasi fulani nje ya mliyokubaliana awali. Maana kama mimi jamaa alikuja akaniambia nimuongee 150,000/= kwenye makubaliano yetu ya awali nikamwambia akwende zake maana tulishakubaliana baada ya yeye kuwa ameangalia michoro na kutathmini kazi yote

Kama alivyosema mdau hapo juu, usimamizi ni muhimu sana. Kwa mfano mimi nilipoamua kuwa sasa napandisha na nikiwa tayari nimeshajipanga ilinilazimu nichukue likizo ofisini kusimamia na kwa kweli sijisifu lakini nilijitahidi kupiga zero distance na nina ujasiri wa kusema fundi hakuniibia hata kidogo....

Usisahau pia wahenga walisema, kabla hujaanza mbio ziulize nyonga kama ziko tayari kwa urefu wa mbio hizo...ukiona nyonga haikupi matumaini, lower your expectations and instead of vying for long jump, just go for short jump....hope umenipata brodaa
 
Mil 20???? Haitoshi ila ni nzuri kuanzia. Ila inategemea kiwanja chako kipo wapi. Kama ni kwenye slope utashangaa...inaweza kuishia kwenye jamvi.

Cha msingi ni control ya nondo na cement....maana cement inalika kweli kweli

Sehemu nyingine tamu ni slub....unaweza imba haleluuuuiiiyaaaaaa....

Ila anza ujenzi usiogope...mdogo mdogo utafika

Ahsante mkuu kwa ushauri. Nachoweza kusema nimegawanya ujenzi huu katika phase nne.
Phase 1 ni kuanzia msingi,kwenda juu na kupaua. Hapa hakuna madirisha wala plaster wala milango. Hapa tu kwanza !!
Phase 2 ndio milango finishing njee nk
 
20M dollor au Tsh? angalia usije ukaenda kitanzini bure!
 
Nashukuru kwa ushauri wako murua Cathode Rays

Katika malipo ya mafundi hapo umeongelea malipo kwa asilimia ila hujasema kutoka wapi? Kwahio unamaanisha gharama za nyumba ni sawa na gharama za fundi manaa ulimlipa mara 25%*4 =100% je hii ndio gharama ya fundi relative to gharama ya ujenzi? Naona kuna kitu sio sawa hapa. Kiwanja changu kipo boko na kipo flat vizuri

Kingine, nimeona kujenga maana sihitaji tena kuja kujenga na kuhangaika kwahesabu zangu najua kwa miaka miwili nitatumia sio chini ya 70M na inaweza isiishe vile navyotaka.

Nashukuru kwa maoni mkuu
 
Last edited by a moderator:
Milioni 20 haitoshi msingi hadi kupaua.
Ila itakusogeza msingi labda na ground floor kwa hatua kadhaa ( kama kiwanja kipo pazuri na usimamizi?, ingawa nina mashaka kwenye jamvi malighafi zitaendaje ktk kujazilizia... unless upo nje ya dsm)

Slub tu material ambayo hayatotumika yanaweza zidi hiyo 20 m (still inategemea na sqm za nyumba yako; maana marine board moja tu inarange kati ya 58,000-60,000 hapa hatujaangalia kushuka kwa shilingi)

Mradi umeamua kujenga ghorofa kaza roho jiandae...... ukiweza jamvi....kunyanyua rahisi kashehse ni slub na paa.

Kumbuka inategemea na aina ya bati pia....inaweza fika tena hiyo 20m kutegemea na unachotumia bati la kawaida, kiboko au za nabaki afrika

Usiangalie sana gharama angalia kujenga nyumba ya ndoto zako. Mradi uwe na uwezo wa kukusanya hela kila baada ya muda fukani na kuendelea na hatua inayofuata ya ujenzi.

Mwisho kama upo kwenye viwanja vilivyopimwa (sijui kwa visivyopimwa) usisahau kibali cha ujenzi toka halmashauri na stika toka bodi (hawa wa stika wasumbufu kama huna watataka kukugeuza mradi)

All the best

Ahsante mkuu kwa ushauri. Nachoweza kusema nimegawanya ujenzi huu katika phase nne.
Phase 1 ni kuanzia msingi,kwenda juu na kupaua. Hapa hakuna madirisha wala plaster wala milango. Hapa tu kwanza !!
Phase 2 ndio milango finishing njee nk
 
Bwana Cathode rays huwezi kujua 20m itakufikisha wapi bila kufanya mahesabu kitaalam. Kwa hapo unapotaka kufikia kwa phase one nakushauri utafute mtaalam afanye hesabu ya vitu vinavyohotajika kwa phase hiyo.

Kwa kutumia michoro uliyo nayo na ikibidi aone na site ilivyo ataweza kukokotoa idadi ya tofali, mchanga, kokoto, nondo, cement, formwork, misumari, ufundi, n.k. Hakika akifanya haya utajua tu hiyo phase unatakiwa uwe na bei ghani.

Period!
 
Hapana mkuu aminiusiamini,

Hapa nimeongelea gharama ya fundi tu... siyo gharama ya ujenzi, ndo maana kwenye maelezo nimesema vifaa nilikuwa nanunua mwenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Bwana Cathode rays huwezi kujua 20m itakufikisha wapi bila kufanya mahesabu kitaalam. Kwa hapo unapotaka kufikia kwa phase one nakushauri utafute mtaalam afanye hesabu ya vitu vinavyohotajika kwa phase hiyo.

Kwa kutumia michoro uliyo nayo na ikibidi aone na site ilivyo ataweza kukokotoa idadi ya tofali, mchanga, kokoto, nondo, cement, formwork, misumari, ufundi, n.k. Hakika akifanya haya utajua tu hiyo phase unatakiwa uwe na bei ghani.

Period!

Samahani mkuu siyo mimi mwenye thread

BTW nakununulia unachosema na cha kwanza mdau anapaswa kufanya ni kuwa na picha halisi ya gharama za ghorofa lake kwa kuwa na BoQ.
Unaweza tafuta mtaalam akakufanyia makadirio baada ya kuangalia mchoro wako (kama aliekuchorea ana utaalamu anaweza kukufaa pia). Unaweza kuingia gharama lakini ni muhimu sana kwa sababu itakusaidia kugawa phases zako kuendana na estimates zilizofanywa....... maana unaweza weka phases nne ambazo jumla zinaleta jumla way less ya actual project cost
 
Back
Top Bottom