Msaada wa kitabibu wa kinywa na meno

Msaada wa kitabibu wa kinywa na meno

Blood of Jesus

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2016
Posts
4,486
Reaction score
8,098
fizi zinaliika, meno yanang'oka. ni ni dawa? najua JF Ina kila mtaalamu

naomba niishie hapo. ninatanguliza shukrani.
 
1. Nenda hospitali.

Kama huna pesa za hospitalini.

1. Piga mswaki kila mara baada ya kula au kunywa vitu vyenye sukari
2. Punguza kula vyakula vyenye sukari hasa sukari ya viwandani.
3. Fizi kuvimba, au mdomo kupata vidonda huweza kusababishwa na aidha bacteria wanaotokana uchafu unaotokana na vyakula anavyokula ambavyo hukusafisha kinywa. Pili, ukosefu wa vitamini hasa Vitamini B12.
Kula matunda.

4. Jiepushe na uvutaji wa sigara
5. Acha kuzama chumvini kama unahiyo tabia
 
Mimi nilikuwa na tatizo kwenye fizi yaani unakuta zimeachia kwenye meno, ukipiga mswaki au ukila chakula kigumu kidogo zinatoa damu.

Nilienda hospital nikaandikiwa nitumie Ascobic acid hivi ni vidonge vya vitamin C .Baada ya kutumia kwa muda tatizo limeisha kabisa .

Ila hiyo kesi ya meno ungeenda tu hospital inaweza kuwa ishu ya kitaalamu zaidi

Sent from my SM-A025U using JamiiForums mobile app
 
Weka picha tukufanyie uangalizi wa tatizo lakosasa ukisema tu bila picha tunafanyaje uangalizi huo ugonjwa imekuaje, weka picha kwanza alafu nikupe majibu nini ufanye

DR Mambo Jambo
Nachomshauri aende hospitali..
Maana unaweza kusema ni Dental Caries Kumbe ni Periodontal D'se..
Au ni scurvy kabisa..
Aende hospitali afanyiwe uchunguzi ili waweze kudadavue
CC: Blood of Jesus
 
asanteni wadau. Hadi sasa nimepata nuru flani kupitia michango yenu. nawasubiri wengine ama nyongeza
 
Mimi nilikuwa na tatizo kwenye fizi yaani unakuta zimeachia kwenye meno, ukipiga mswaki au ukila chakula kigumu kidogo zinatoa damu.

Nilienda hospital nikaandikiwa nitumie Ascobic acid hivi ni vidonge vya vitamin C .Baada ya kutumia kwa muda tatizo limeisha kabisa .

Ila hiyo kesi ya meno ungeenda tu hospital inaweza kuwa ishu ya kitaalamu zaidi

Sent from my SM-A025U using JamiiForums mobile app
habari,kuna mtu kapost ktk thread flani kuwa una story inayohusu mambo ya uchawi,naomba unitag ktk thread husika,ubarikiwe
 
Back
Top Bottom