Msaada wa kiufundi kwenye iPhone 7

Joined
Sep 8, 2017
Posts
60
Reaction score
266
Habari

Kwenye iphone kuna kitu kinaitwa switch control sasa kimetokea na sasa simu imeshaji lock nahitaji kuingia kwa passcode ila nashindwa

ukitaka kuanza kuandika passcode tu inatokea mistari ya blue kama inavyoonekana hapo chini imezunguka passcode

na nikubonyeza namba ina pop up kitu kama hiki hapa chini



sijui namna gani nitaweza kuingia bila hili tatizo ili niende kwenye setting kuondoa hiyo switch control

shida nyingine inakujaa home button haifanyi kazi

hapa nikitaka kuslide inaniletea hiyo strip ya blue



Msaada jama kama kuna namna yoyote
Yaani ni kama touch haisense kitu chochote
 
Mkuu switch model ni Accessibility setting most of times hizi ni features za walemavu, ama watu wanaohitaji msaada zaidi.

Nimecheki site Ya Apple unaweza kuiswitch off kwa kubonyeza home button mara 3 haraka haraka, ama sometime bonyeza side button mara 3 ikiwa huna Home button.

Tembelea hapa kwa maelezo zaidi
 

Bonyeza home button mara tatu haraka haraka โ€ฆ.itatoka boss
 
Kama home button haifanyi basi u need to replace it
 
Ningeiokota hiyo simu ikiwa hivyo cha kwanza ningehisi hiyo simu display imepasuka, na ningetouch ingenigomea ningeconclude simu imeharibika display na touch.

So nafikiri siyo kwamba haisense kwa sababu ya hiyo feature ila ni kwavile simu imeharibika display na touch. Ingekua hiyo feature ya ulemavu na sense zingekua nzima ingekua inakupa taarifa ya unachogusa.
 
Daaaaah, broo bado upo jfm, maana kitambo sana sijaona nyuzi zako za ukweli mambo ya code, programingi nk, mpaka niliwahi kuuliza huyu jamaa alipotelea wapi,
๐๐ข ๐Š๐ก๐ž๐ซ๐ข ๐ฅ๐š๐ค๐ข๐ง๐ข ๐ฆ๐ค๐ฎ๐ฎ
 
Kheri mkuu
 
Mkuu ulipata ufumbuzi?

Kama bado ngoja njiazie nyama kwa Chief Mkwawa.

Kama home batani haifanyi kazi jaribu hii mbinu,

=>Gusa sehemu unayotaka kuingia iki-highlight (ikionyesha kwa kuzungushia ule msitari wa buluu) sehemu husika uta...,

=>Hatua inayofuata uta-double click sehemu iliyozungushiwa mstari (utagusa sehemu husika mara mbili harakaharaka(mfululizo)).
Mfano hapo kwenye passcode we unagusa namba stahiki ikizungushiwa mtari wa buluu una gusa mara mbili mfululizo itakubali utaendelea hivyo hivyo hadi utapofika kwenye voice over feature ndani ya SETTING.

=>Ukihitaji ku-scroll juu au chini utatakiwa utumie vidole vitatu kwa pamoja visipishane, utaona inafanya kazi kama kawaida, ukitumia kidole kimoja haikubali, utafanya hivyo mpaka utakapofika ndani ya setting na kubadilisha.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ