Hapa hakuna sheria inayokubana alipe yeye mwenyewe usitoe hata senti.LKN pia anataka nimlipie kodi ya nyumba yake atakayo hamia yeye kama yeye sababu mtoto atakuwa tayari shule na anasema nisipo fanya hivyo anaenda kwenye sheria.
lkn bahati mbaya au nzuri huyu mwenzangu alikuwa kaokoka. na akawa anadai kuwa kama nataka kumuoa basi tukafunge harusi kanisani kwao ambalo ni kanisa la kilokole.
Sasa yeye anategemea nini? Wewe kama una ndugu zako au wengine unaoona wanafaa we waite wakae na mtoto.Mkuu ni kwamba hataki mtoto akae na mtu yoyote si mama si dada wala nani... na yeye anasema atakuwa busy so option pekee aliyonipa ni kupeleka mtoto shule. hata mimi naona mtoto bado ni mdogo ila sina cha kufanya.
nimeishi na huyu mwanamke kwa mda wa miezi 11, na tayari nilikuwa nimezaa naye kabla ya hapo, mtoto wetu ana miaka mitatu sasa. kisa kilichotokea ni kwamba mwezi wa saba tulikuwa tunajadili kufunga ndoa ili tukae kihalali kwa maana ya misingi ya DINI.
lkn bahati mbaya au nzuri huyu mwenzangu alikuwa kaokoka. na akawa anadai kuwa kama nataka kumuoa basi tukafunge harusi kanisani kwao ambalo ni kanisa la kilokole. mimi nasali lutherani na yeye before alikuwa anasali lutherani pamoja na wazazi weu wote wanasali lutherani, ubishi ulienda mpaka ikafikia harusi kuahilishwa na ikabidi tutengane.
Hapa ndio ugomvi unapotokea yeye anasema kwa kuwa anahama basi mtoto wetu wa miaka mitatu tumpeleke shule ya bodding kwa sababu na yeye anafanya kazi hivyo itakuwa busy. nimekubaliana naye na gharama za kumpeleka mtoto shule ntatoa kwa aslimia 100.
Gharama za kumludisha mfanya kazi wetu wa ndani ambaye anatoka mbeya pamoja na kumlipa angalau ahsante ya kukaa naye pamoja ntaghalamia mimi kwa asilimia 100.
LKN pia anataka nimlipie kodi ya nyumba yake atakayo hamia yeye kama yeye sababu mtoto atakuwa tayari shule na anasema nisipo fanya hivyo anaenda kwenye sheria ili niweze kukidhi haja zake. kumbuka kuwa mshahara wangu na wake wa kwake ndio mkubwa. naomba ufafanuzi wa kisheria je ninapaswa kufanya haya yote kwa huyu mama tunaye achana, ambaye hata ndoa hatukufunga bado.
(II) Umeishi na huyu mama kwa miezi 11 ambayo haitimii miezi 24 ambayo sheria inaashiria ndoa (yaani Presumption of marriage) katika kifungu 160 cha sheria ya ndoa. Kama mngekuwa mmeishi miaka 2 na kuendelea basi hata kama mlikuwa hamjafunga ndoa kufuatana na maelezo ya (I) hapa juu, sheria ingewatambua kama wanandoa. Na kama mngehitaji kutengana basi ingetakiwa kufuata taratibu za kuachana zilizo orodheshwa kisheria. Kwa hiyo kama anataka kwenda mahakamani atashindwa.
Mkuu kwani mlisha oana?
Usimpangie nyumba utakuwa unachunwa aende kokote.
shost you wil be suprised to hear, siwezi kumsemea huyu kaka kwamba kuna kitu anaficha inawezekana kweli au pia ikawa si kweli ndungu yangu. nimeona kwa macho mama kuna ndugu alianza kwenda kwa kakobe tangu alivyorudi siku ya kwanza alibadilika kitabia mpaka ukawa ugomvi na mumewe na ikaishia kutengana coz wote waislam sasa anamlazimisha mumewe awe mlokole imekaaje hiyo? mwenzangu hawa watu wakiiingia kwenye hiyo dini wanakuwa hawashikiki , balaaa lake si dogo.so wala simshangai huyu kaka zaidi nampa pole na bora waachane tu maana huyo keshakuwa obsessed na hazinduki leo.na nyie msiwe mnaendeshwa kama magari ya dubai au ya japani ovyo eti kisa umelipia MV au insurance.
I wish to see that lady.Ni wa ajabu hata sijawahi kuona anajivunia nini kwa kumtreat mwenzie hivyo?
Anyway kwa kumlazimisha huyo bwanae amlipie kodi ya nyumba wakati hawapo pamoja na kulazimisha ndo ifungwe kwa kuzingatia ulokole kamwe haileti maana ila ninachodhani kuna kitu hakikusemwa na mleta mada kinachopelekea huo ugomvi.
Ni nini chanzo cha huyo dada kuokoka?
walikubaliana na mzazi mwenza?
Je wakati wanapanga masuala ya kufunga hiyo harusi alikuwa bado kuokoka au hakumshirikisha na uamuzi wa kuokoka?
Jamani tujaribu kuwa na moyo wa utu siku zingine kwa kuwa wote tu viumbe vya mungu huyohuyo./
Kwa nini tyuwapelekesha kwa starehe ya inayowapa raha wote wawili?
acheni kujishusha mtu unapata mshahara mkubwa kuliko mwananume halafu hutumii zako unataka kutoboa mfuko wa mwenzio maana yake nini.
Kikubwa amuweke chini amwambie kila kitu na madhara ya baadae kwa mtoto na wote kwa pamoja na kama mwanamke akipenda kumshitaki mimi nitakuwa wakili kwa upande wa huyo mwananume .
Kwa upande mwingine tumezidi kuwaonea hawa ndugu zetu ilhali ndo waliotoa ubavu wao ili tuwepo duniani.
(I) Kufuatana na Sheria ya Ndoa (Law of Marriage Act, 1971) wewe hujaoana na huyu mama, na huna ulazima kisheria kumtunza yeye. Sheria hii inatambua ndoa aina tatu, (1) civil, yaani ya kiserikali, kama watu wanavyokwenda kwa area commissioner kufunga ndoa, (ii) ndoa inayofungwa kidini, kama vile kanisani au msikitini (iii) ndoa iliyofungwa kwa mila ya desturi - kitamaduni. Kufuatana na uliyosema hapa, wewe hukufanya yeyote haya matatu. (angalia kifungu 25 cha sheria ya ndoa, 1971)
(II) Umeishi na huyu mama kwa miezi 11 ambayo haitimii miezi 24 ambayo sheria inaashiria ndoa (yaani Presumption of marriage) katika kifungu 160 cha sheria ya ndoa. Kama mngekuwa mmeishi miaka 2 na kuendelea basi hata kama mlikuwa hamjafunga ndoa kufuatana na maelezo ya (I) hapa juu, sheria ingewatambua kama wanandoa. Na kama mngehitaji kutengana basi ingetakiwa kufuata taratibu za kuachana zilizo orodheshwa kisheria. Kwa hiyo kama anataka kwenda mahakamani atashindwa.
(III) Haimanishi basi kwamba huna majukumu yeyote kwa matunzo ya mtoto wako. Unasema wewe una kipato kikubwa kuliko mama wa mtoto wako, kwa hiyo kisheria unatakiwa kutoa matunzo. Sheria inayoitwa Affiliation Ordinance inampa hakimu uwezo wa kutoa summons kama ataridhishwa kwa wewe ni baba wa mtoto (Affiliation Ordinance Act, 1964, kifungu cha 4) kwa hiyo kama ukikataa kutoa matunzo ya mtoto wako, unaweza kufikishwa mahakamani na kulazimishwa kutoa matunzo ya mwanao.
Nadhani hii imekupa mwanga kidogo wa nini cha kufanya.