Msaada wa kubadili herufi katika kitambulisho cha taifa.

Ufwandunkanye

Senior Member
Joined
Jan 7, 2017
Posts
123
Reaction score
193
Tafadhari, kama kichwa kinavyosema.

Nina kitabulisho cha taifa nilijiandikishia Dar ila kwa sasa nipo mkoani. Lakini nilipochukua niliangalia picha na majina juu juu na kuweka sahihi na kuondoka kwa sababu ya kuchoka kufuatilia na foleni. Lakini baadae nikagundua kwamba kuna herufi imekosewa katka jina la katikati.

Sasa naombeni kujuzwa. Je, naweza kurudi Dar kukirekebisha au nikarekebishia mkoani? Na je, muda wa marekebisho unaweza kuwa kama kusubiri kitambulisho kipya? Na je, nitahitajika kubeba documents zote? Msaada tafadhari.

Nitashukuru kwa msaada wenu.
 
Kama kina picha yako achana nako utabadilisha siku una renew
 
Ninakushauri uende ukafanye marekebisho. Andaa nyaraka zote ulizozitumia mwanzoni na kiasi cha Tsh. 20,000/-
 
Yani jina la kwanza liko sawa latatu liko sawa picha ni yako unaangaikaje na kosa la herufi moja
 
Ninakushauri uende ukafanye marekebisho. Andaa nyaraka zote ulizozitumia mwanzoni na kiasi cha Tsh. 20,000/-
Pia awe na kitambulisho chenye majina yake sahihi ( kama kitambulisho cha mpiga kura). Muda wa kukisubiri inaweza kufika hadi wiki 4-6.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…