Msaada wa kuishitaki serikali kwa matokeo mabaya ya kidato cha nne 2010.

Msaada wa kuishitaki serikali kwa matokeo mabaya ya kidato cha nne 2010.

Vitendo

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2009
Posts
582
Reaction score
103
Ndugu wanaJF ninaomba msaada wa kisheria ili kufungua kesi ambayo nalenga washitakiwa kuwa ni wafuatao.
1)IKULU.
Rais wa Tanzania aliishahuri wibaya wizara ya elimu kuondoa mtihani wa kidato cha pili na hiyo imetajwa kuwa ni moja ya sababu ya ufaulu kushuka kwa 22%.
2)Wizara ya Elimu
Kushindwa kusimamia elimu.
3)Ofisi ya waziri Mkuu,tawala za mikoa na serikali za mitaa ..hawa wanawajibu katika shule leo hii tunazoziita za KATA.

ukiangalia matokeo yanatia huzuni na huruma pia.

DARAJA I WANAFUNZI 5363
DARAJA II WANAFUNZI 9942
DARAJA III WANAFUNZI 25083
DARAJA IV WANAFUNZI 136,633
DARAJA 0 WANAFUNZI 174,193
Mimi naamini serikali na vyombo vyake walikuwa/wana uwezo wa kudhibiti maafa haya ila kwa makusudi kabisa wameacha yametokea.
Hivyo basi yeyote aliyeko tayari kunipa msaada wa kufungua kesi hii naomba tuanze mchakato mara mmoja maana hii ni kuharibu mustakabari wa taifa letu.
asante.
 
Shida ni kwamba ukiishitaji, alafu ukalipwa fidia ni pesa zetu wenyewe ndio zitawalipa..., Aaargh, Its a no win situation, anyway kama ukitaka kuwashitaki wahusika.. (individuals) na sio serikali mimi takuunga mkono..., tena wewe ukishinda kesi ni nyingi tu zitafata, sababu ni mengi waliyochakachua
 
Unawashtaki ukiwa kama nani? Au na wewe ni mmojawapo wa waliopata zero?
 
Halafu ndio Mr. Ahadi anawahakikishia watz kuwa mtashindana na wenzenu kwene EAC?? amin nawaambieni, hata kama kupata kazi za kuosha madishi au kuwa walinzi kijasho kitawatoka...achilia mbali kazi zinazohitaji ujuzi mkubwa.

Unajua nakumbuka ktk mishemishe flani nlifika ubalozi flani, mlinzi kudadeki analonga kingilishi chenye lafudhi ya kikenya, na hiyo was long time ago, na uhakika tuendako wabongo watakuwa hawana chao tena hata huko kwene ulinzi, na kazi nyingine manual kama hizo.

Its official, taifa la wazembe, wajinga na wapumbavu.
 
Ndugu wanaJF ninaomba msaada wa kisheria ili kufungua kesi ambayo nalenga washitakiwa kuwa ni wafuatao.
1)IKULU.
Rais wa Tanzania aliishahuri wibaya wizara ya elimu kuondoa mtihani wa kidato cha pili na hiyo imetajwa kuwa ni moja ya sababu ya ufaulu kushuka kwa 22%.
2)Wizara ya Elimu
Kushindwa kusimamia elimu.
3)Ofisi ya waziri Mkuu,tawala za mikoa na serikali za mitaa ..hawa wanawajibu katika shule leo hii tunazoziita za KATA.

ukiangalia matokeo yanatia huzuni na huruma pia.

DARAJA I WANAFUNZI 5363
DARAJA II WANAFUNZI 9942
DARAJA III WANAFUNZI 25083
DARAJA IV WANAFUNZI 136,633
DARAJA 0 WANAFUNZI 174,193
Mimi naamini serikali na vyombo vyake walikuwa/wana uwezo wa kudhibiti maafa haya ila kwa makusudi kabisa wameacha yametokea.
Hivyo basi yeyote aliyeko tayari kunipa msaada wa kufungua kesi hii naomba tuanze mchakato mara mmoja maana hii ni kuharibu mustakabari wa taifa letu.
asante.

Changamoto zuri sana, tuanzie hapa kwenye Katiba yetu. Katiba yetu inasema kuwa malengo muhimu na misingi ya mwelekeo wa shughuli za umma ni pamoja na:
(1) Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa haki ya mtu kufanya kazi, haki ya kujipatia elimu na haki ya kupata msaada kutoka kwa jamii wakati wa uzee, maradhi au hali ya ulemavu, na katika hali nyinginezo za mtu kuwa hajiwezi. Na bila ya kuathiri haki hizo, Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa kuhakikisha kwamba kila mtu anaishi kwa jasho lake.
(2) Kila mtu anayo haki ya kujielimisha, na kila raia atakuwa huru kutafuta elimu katika fani anayopenda hadi kufikia upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake.

Kwa hiyo wanavyosema haki ya kupata elimu ina maana kupata elimu bora na nzuri, sio kufeli. Kwa misingi kiyo kusomesha watoto kwenye shule zilizo chini ya kiwango ni kwenda kinyume cha katiba yetu.
Ingawa ibara ya 7 (2) ya katiba inakataza mahakama kukazia haki iliyomo kwenye isehemu hii lakini mahakama za nchi nyingine zinasisitiza kuwa malengo ya katika ni muhimu kama zilivyo haki na wajibu kwani malengo ya katika ni msingi wa yote yaliyomo kwenye katiba.

waone watu wa Kituo cha sheria na haki za binadamu au ktuo cha msaada wa sheria (NOLA) wanaweza kukupokea kwa mikono miwili.
 
Back
Top Bottom