MSAADA: wa kujua bei za vifaa hivi

MSAADA: wa kujua bei za vifaa hivi

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,753
Reaction score
9,575
Habari wanajf

Natumai mko fiti na mnaendelea na shughuli zenu

Naitaji mnisaidie bei za vifaa hivi kwani nataka kuvinunua kwa ajili ya biashara yangu ambayo nataka kuifugua hivi karibuni sasa sijui bei yake acha niwaorodhoshee vifaa vyenyewe.

a) Sewing Machine aina ya Butterfly made in Thailand, India nk na sio china
b) Embroidery Machine aina ya Butterfly
c) Screening Machine ya kuprint
d) Offset machine aina ya GTO, TOK, Haiderbag made in Thailand, Usa, uingereza
e) Scanner kubwa ya kutoa photo picture
f) na UPS

Nashukuru sana kwa msaada wenu mnakaribishwa kunisaidia kwa mambo hayo niliyoyataja.
 
Kwanini sio China dada? Tatizo watu tunaoishi bongo tunadanganyika kuwa kitu kikitoka china ni fake au low quality kumbe we r definitely wrong, china unapata bidhaa kutoka na pesa ulionayo, mchina anatengeneza kitu kuangalia uwezo wa pesa ya mtu, me ninaishi China dada ndio maana nakuambia hivyo, huku ukitaka fake unapata na original unapata, na pia kuna vile vimeo kabisaaaaaa hata huku katika maduka ya kichina haviruhusiwi kuuzwa kwn serikali haija idhinisha viwekwe madukani, sasa hivyo ndio tunaletewa huko Africa, mchina mwenyewe hata bure hatumii, mfano mmoja dada nasikia bongo sijui kuna simu zinaitwa sijui Techno zinatoka huku china, me maisha yangu yote ya huku sijawahi kuziona madukani au hata kumuona mchina anatumia simu ya jina hilo, nasikia bongo zimejaa kinomaaaa, hizo simu zinaletwa huko kwani ni za bei chee, ndio maana unaweza kukuta tunapata matatizo ya kiafya bongo kwa vitu km hivyo dada, sasa simu haina kiwango cha kutumia binadamu lkn inauzwa mtu anaweka sikioni wkt simu ni mambo ya radiation, mtu unaweza ht kupata cancer, samahani kwa kukuchosha na gazeti dada,
 
Acha kudanganya watu kwamba TECNO ni simu fake hebu tuambie simu original za Tanzania basi au ni kupondea.
kwa Taarifa TECNO Hawauzi simu zao Tanzania pekee, jaribu ku google uone masoko yao.
 
Back
Top Bottom