Msaada wa kupata daktari

MNDEE

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2009
Posts
491
Reaction score
68
Wanajamvi, natafuta second opinion ya daktari mtaalamu wa spinal na back pain Tanzania. Kama wewe ni daktari au unamfaham daktari au una experience na huu ugonjwa nahitaji contact na ushauri.

Symtoms za mgonjwa ni maumivu makali yakianzia lower part ya mgongo na kushuka mguu mmoja. Maumivu yanapungua mgonjwa anapokuwa amelala au kukaa. Kusimama ni shida na kutembea ndio kabisa tatizo limeanza about two weeks ago (mgonjwa hajaanguka wala hajapata ajali). Amefanyiwa x-ray na kuambiwa kuna disc 'zimesimama' na akawa prescribed sindano (bahati mbaya sina jina la dawa) lakini maumivu bado yapo pale pale.

Nimegoogle basing on symptoms magonjwa aina mbili naona symptoms zinafanana Herniated disk na Spinal Stenosis. Tafadhali kama unamfaham daktari au una ushauri naomba uwasiliane nami kwenye hii thread au unaweza ni PM, thanks.
 
Mpeleke MOI muhimbili, utawapata waliobobea, kwa huduma nzuri na haraka jiandikishe kuingia kiliniki ya daraja la kwanza.
 
Mpeleke MOI muhimbili, utawapata waliobobea, kwa huduma nzuri na haraka jiandikishe kuingia kiliniki ya daraja la kwanza.

Mkuu ahsante kwa ushauri.
 
Hapo utampata Dr Kinasha mtaalamu aliyebobea kwa maswala hayo hamna mwingine wa calibre yake Tanzania

Mpeleke MOI muhimbili, utawapata waliobobea, kwa huduma nzuri na haraka jiandikishe kuingia kiliniki ya daraja la kwanza.
 
Mpeleke MOI muhimbili, utawapata waliobobea, kwa huduma nzuri na haraka jiandikishe kuingia kiliniki ya daraja la kwanza.

Ndugu yangu! Kama una pesa nenda India, ni kweli tunao hapa lakini sitaki kuharibu sifa ya watu...

La ukishindwa basi itabidi uende pale kuna mabingwa Kama huyo Kinasha na vijana waliofuzu kutoka sauzi hivi karibuni ambao ni wazuri
 
Hapo utampata Dr Kinasha mtaalamu aliyebobea kwa maswala hayo hamna mwingine wa calibre yake Tanzania

Mzuzu ahsante kwa kunipatia hili jina la huyu daktari.
 
Ndugu yangu! Kama una pesa nenda India, ni kweli tunao hapa lakini sitaki kuharibu sifa ya watu...

La ukishindwa basi itabidi uende pale kuna mabingwa Kama huyo Kinasha na vijana waliofuzu kutoka sauzi hivi karibuni ambao ni wazuri

Mkuu hawa watalaam wakituambia matibabu yanayotakiwa ni surgery taratibu nyingine zitafuata. Mgonjwa yuko kwenye 70s ukimsubject kwenye surgery itabidi iwe sehemu ambayo success is 99%. Wazee wa US hii ngoma emergency room mnaonaje!
 
Mpeleke India ...my dad alipata tatizo kama ilo since 2001 mpaka Leo hajatembea...na alikutana na huyo huyo...kinasha akamfanyia surgery.. Ila kama pesa tatizo kama mwenzangu na Mimi...nenda tu MOI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…