MSAADA WA KUPATA NYUMBA YA KUPANGA ZA NHC DAR ES SALAAM

Joined
May 22, 2017
Posts
74
Reaction score
33
Habari wanajamii forum,
Naomba msaada wa kusaidiwa kupata nyumba ya kupanga za NHC Dar es salaam eneo laweza kuwa Ubungo Shekilango au eneo lolote ambalo litanirahishia kufika hospitali ya muhimbili kwa urahisi kwani kwa sasa nauguza Mgonjwa ambaye anilazimu kumpeleka kwenye session muhimbili Mara 3 kwa wiki. Kutokana na sababu hii gharama zimekuwa juu kiasi kwamba kukosa kumpeleka baadhi ya session.

Kwa msaada, maelekezo au taarifa yoyote ambayo Tanesha kupata nyumba ya NHC.Mawasiliano yangu

Namba:0655428658/0783262125
 
Ukipata hizo nyumba niitwe kuku,kabla mtu hajatoka kwenye hizo nyumba ana muuzia mwingine kwa gharama kubwa.
 
Pole sana na kuuguza mkuu.

Tatizo kubwa Tanzania mambo yanafuata kujuana, si mfumo.

Kuna aunt yangu mmoja alirudi Tanzania kutoka nje baada ya kukaa miaka mingi.

Akawa anatafuta nyumba za NHC. Badala ya kuuliza mchakato gani ufuatwe ili apate nyumba, alijiuliza anamjua nani NHC, akajua anamjua Mkurugenzi Mkuu, akaenda moja kwa moja kwa Mkurugenzi Mkuu, akapata nyumba Masaki.

Ukienda wewe kufuata mfumo unaweza kusota miaka hujapata nyumba, na nyumba zipo kila siku watu wanapata. Unaona huyu mtoto wa Waziri gani kapata nyumba, yule anajuana na mstaafu mzito fulani kapata.

Mimi nilikuwa nakaa hapo karibu kabisa na Muhimbili Hospital nilikuwa naichukulia hiyo sehemu poa sana, lakini sasa naona ni sehemu muhimu sana.

Jaribu kutafuta habari kutoka NHC labda utapata nafasi, lakini izoefu wangu na habari zao, japo wa muda kidogo, ni mbaya.

Sijui kama siku hizi wamebadilika.
 
Anza kwa kuuliza wenye mamlaka mkuu hao NHC, hata mimi nazitolea udenda hizo nyumba zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…