Msaada wa kupata taarifa za investor(s) wa kibiashara

Msaada wa kupata taarifa za investor(s) wa kibiashara

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
1,013
Reaction score
1,183
Habari za muda huu.
Napenda kuja kwenu kwa mara nyingine tena, baada ya kufanya marekebisho ya mpango wa biashara (business plan) nahitaji mwekezaji ambaye atanipatia mkopo wa $ 332,825 nataka kuwekeza kwenye mradi wa kutengeneza nguo namaanisha (Clothing line production) ila itakuwa ni mradi mdogo (small scale business). Tutaingia nae makubaiano kuwa faida itakayopatikana kwa mwaka nitampa 20% (profit sharing per year) na nitarejesha mtaji wake ndani ya miaka 5.
Baada ya kupitia ushauri wa watu mbalimbali nimeamua kuweka mradi huu uwe rafiki kwa mazingira ya nchi. Kupitia mradi huu nitaweza kuajiri vijana wengi, kuiwezesha serikali mapato na kusaidia watu wengine kuwawezesha kupitia biashara hii maana itaunganisha watu wengi zaidi nje na mradi husika namaanisha kibiashara kulingana na mikakati ya kibiashara iliyopo.
Kwa ambaye yupo tayari na anania njema ya kunifanya niweze kutengeneza hicho kiwanda namkaribisha aje anisaidie kwa kunipatia taarifa za fedha, kuniunganisha na mwekezaji binafsi au mwekezaji kampuni.
Endapo akipatikana mwekezaji nitamwonyesha mradi kupitia nakala husika(business plan documented). Kwa ambaye mwenye uwezo au ufahamu naomba aje PM tulijenge taifa.
Asanteni sana na Mungu awabariki.
 
njoo pm then utume details za biashara yako nijue nakusaidiaje
 
Back
Top Bottom