Ozzie
JF-Expert Member
- Oct 9, 2007
- 3,217
- 1,261
Nina PDA aina ya ASUS mypal A626 ambayo haina sehemu ya kupachika SIM card. Kwa sasa ninaweza nikaitumia sehemu yoyote penye Wi-Fi au Wireless network yeyote ile. Ningependa niitumie kwa internet ya kampuni za simu za mkononi kama Zantel au Vodacom kama tufanyavyo kwa simu za mkononi. Nijuavyo mimi kuna namna kampuni ya simu husika yaweza kuipa namba bila SIM card kama baadhi ya modem za Zantel ambazo huwa zinapewa namba bila kuweka SIM card. Maana nilipita nayo kwenye Voda na Zantel shops za mkoa mmojawapo pembezoni mwa nchi yetu wakaniambia labda Voda au Zantel makao makuu wanaweza kunisaidia. Hivi yawezekana kwa Tanzania?