Msaada wa kuuza deni kwa haraka 30 mln

Msaada wa kuuza deni kwa haraka 30 mln

Silicon Valley

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2012
Posts
1,092
Reaction score
1,118
MSAADA WA KUUZA DENI KWA HARAKA 30 mln
Tunafanya biashara ya kukopesha pesa kwa Riba, Pana wateja wetu tunaowadai na bahati mbaya na sisi tumejikuta tuna mapungufu ya pesa kwa haraka pia tokana na mikataba yetu na wateja inahitaji kusubiri kama mwezi mmoja tu, tumeongea na mteja mmoja amekubali kuhamia popote hilo deni lake ili sisi tuuze na tuweze kupata hizo peta,, tafadhali kwa yeyote alie tayari atujulishe na tutamuachia faida ya kutosha kutoka kwa mkataba huo
 
Dah ...Subiri wanakuja wenyewe...
 
Attachments

  • 1403261408904.jpg
    1403261408904.jpg
    27.2 KB · Views: 332
MSAADA WA KUUZA DENI KWA HARAKA 30 mln
Tunafanya biashara ya kukopesha pesa kwa Riba, Pana wateja wetu tunaowadai na bahati mbaya na sisi tumejikuta tuna mapungufu ya pesa kwa haraka pia tokana na mikataba yetu na wateja inahitaji kusubiri kama mwezi mmoja tu, tumeongea na mteja mmoja amekubali kuhamia popote hilo deni lake ili sisi tuuze na tuweze kupata hizo peta,, tafadhali kwa yeyote alie tayari atujulishe na tutamuachia faida ya kutosha kutoka kwa mkataba huo

We mwenyewe ukisoma hii kitu unaielewa?
 
We mwenyewe ukisoma hii kitu unaielewa?

Yawezekana kweli usielewe na hasa kama huna mwanga wa shughuli za biashara za kifedha, pia mm sina taaluma ya utoaji wa habari au taarifa, nasikitika lakini kama uko lnterested ni PM, kwa ufupi tunauza mkataba wa Deni tulilomkopesha mtu/mteja badala ya kusubili atulipe yeye wewe utulipe kwa kulinunua kwa pungufu kidogo ya zile mteja atakazolipa. muda ukiwadia atakulipa wewe moja kwa moja. kwani wewe utakuwa ulishatulipa/nunua kwetu
 
Mnafanya biashara ya riba/kukopeshana,je mmejisajili kisheria?
Sheria zetu zinaruhusu mtu binafsi kufanya biashara ya riba?
Labda kama ni taasisi inayotambulika kisheria.
 
Ni taasisi iliyosajiriwa kisheria na inazo office zake hapa mjini
 
mnafanya biashara ya riba/kukopeshana,je mmejisajili kisheria?
Sheria zetu zinaruhusu mtu binafsi kufanya biashara ya riba?
Labda kama ni taasisi inayotambulika kisheria.

hapo ndio utajua kuna harufu ya utapeli.
Iweje taasisi imuuzie mtu binafsi deni?
Sheria za nchi zinasemaje?
Je sheria za taasisi yao zinaruhusu hilo?
Kama ni taasisi ilosajiliwa na hainamatatizo; kwanini wasiende bank kukopa kama wanauhitaji wa hela?
 
Jamaa lazima watakua from Lumumba.
 
mnauza majanga,mmeshindwa kudai watu mnataka kuwaingiza mkenge raia.

huu ni utapeli wa wazi wazi eti ununue deni uanze kumdai mtu ambaye ukumkopesha wewe na wala humjui kudadadeki damn
 
tumewashtukia; iweje taasisi ilosajiliwa tena inayohusika na utowaji mikopo iogope KWENDA bank kukopa ije itafute watu binafsi wa kuukopesha tena fedha zenyewe ndogo kama mil 30?

Kama mnakopa mil 30 kwa watu binafsi mnamtaji wa shilling ngapi?
 
MSAADA WA KUUZA DENI KWA HARAKA 30 mln
Tunafanya biashara ya kukopesha pesa kwa Riba, Pana wateja wetu tunaowadai na bahati mbaya na sisi tumejikuta tuna mapungufu ya pesa kwa haraka pia tokana na mikataba yetu na wateja inahitaji kusubiri kama mwezi mmoja tu, tumeongea na mteja mmoja amekubali kuhamia popote hilo deni lake ili sisi tuuze na tuweze kupata hizo peta,, tafadhali kwa yeyote alie tayari atujulishe na tutamuachia faida ya kutosha kutoka kwa mkataba huo
Yeye atafahamishwa kua kuanzia leo anadaiwa na mimi na sio nyinyi!??

Na asiniponilipa nitambana vipi mtu ambae sikumkopesha?

Asiponilipa naruhusiwa kuwadai nyinyi?

Nyinyi niwape 30mil, then yeye atanilipa ngapi?
 
Kwanza : Ni biashara ya kawaida sana kununua madeni labda hapa kwetu haijashamiri watu wengi kuielewa, pia ni kawaida sana mtu kuhamisha mkopo wake toka banki(microfinance) moja hadi nyingine kwa sababu tofauti tofauti ni pamoja na hiyo ya kuuza madeni,

Pili : Ni kwa vile huwezi kuaandika maelezo yote hapa ili kukidhi kuwaelimisha na pia kuaondolea mashaka hapa hadi kila mmoja wetu kuelewa na kulidhika kuwa ni shughuli za kibiashara za wazi na halali hakuna niya yeyote mbaya wala dalili za utapeli hata chembe, kila bidhaa muuzaji lazima ashawishi wanunuzi.

Tatu: Sio kweli kwamba sisi tumeshindwa kukopa Bank nadhani sote tunajua taratibu za mabanki yetu yalivyo hasa panapo hitajika swala la HARAKA. TUNAOMBA RADHI KAMA SWALA HILI LIMEWAKWAZA SIO NIA YETU...
 
Yeye atafahamishwa kua kuanzia leo anadaiwa na mimi na sio nyinyi!??

Na asiniponilipa nitambana vipi mtu ambae sikumkopesha?

Asiponilipa naruhusiwa kuwadai nyinyi?

Nyinyi niwape 30mil, then yeye atanilipa ngapi?

Taratibu zote kwa Advocate na unapewa power yote na mkataba original na yeye yupo akishuhudia na kusaini kama mdaiwa,

---Asipokulipa kama kawaida unafuata taratibu za kisheria kwa kumchukua broker anatangaza kuuza hadhaani mali iliyowekwa rahani na kuuza (nyumba) na hati unakuwa unayo.

---Deni kamili ni zaidi ya sh 30 mln, kwa ufupi tokana na mkataba huo ndani ya mwezi mmoja hutakosa chini ya 3-4 mln kama faida yako mengi njoo mezani tuongee wote muuzaji, mdaiwa, mnunuzi.
 
kama kweli ni kitu cha halali na kisicho na mashaka; Mbona mnaogopa hata kutaja jina la kampuni na ofisi zenu zilipo?

pili, Mbona zipo benki nyingi tu zenye mikopo ya haraka na tena kwa taasisi Ndio Itakuwa rahisi zaidi kuwakopeasha?

Au mnajiendesha kwa hasara kiasi kwamba hamkopesheki?
 
Yawezekana kweli usielewe na hasa kama huna mwanga wa shughuli za biashara za kifedha, pia mm sina taaluma ya utoaji wa habari au taarifa, nasikitika lakini kama uko lnterested ni PM, kwa ufupi tunauza mkataba wa Deni tulilomkopesha mtu/mteja badala ya kusubili atulipe yeye wewe utulipe kwa kulinunua kwa pungufu kidogo ya zile mteja atakazolipa. muda ukiwadia atakulipa wewe moja kwa moja. kwani wewe utakuwa ulishatulipa/nunua kwetu
kama EPA vile. Ila CCM ndiyo wajuvi wa kununua madeni hewa, kawauzie.
 
Jamani mbona mnamshambulia huyu mleta mada kama hujui kitu nyamaza au uliza ueleweshwe vizuri.kwa ufahamu wangu mdogo hii biashara ya kuuza deni kwa makampuni yanayoitwa DEBT COLLECTION AGENCY or DEBT COLLECTORS.kazi yake kubwa ni Wakala wa kukusanya madeni.mfano;tanesco & dawasco zinawadai watu wengi bill za nyuma ambazo watu walikuwa awalipi kabla ya kuweka system ya luku.alternative tanesco wangeamua kumtafuta debt collector halafu wangemuuzia madeni yote wanayowadai watu ili wao wapate hela yote lumpsum ili iwasaidie kufanya mambo mengine kwa haraka kuliko kuidai taratibu.hawa debt collector wanapata faida pale ambapo labda kama una deni la 30 million unawauzia kwa million 25.kiufupi hii ni biashara halali kabisa hata brela imesajili haya makampuni mfano ni majembe auction mart.katika memorandum yao wameandika pia kampuni yao ni debt collection agency.
 
MSAADA WA KUUZA DENI KWA HARAKA 30 mln
Tunafanya biashara ya kukopesha pesa kwa Riba, Pana wateja wetu tunaowadai na bahati mbaya na sisi tumejikuta tuna mapungufu ya pesa kwa haraka pia tokana na mikataba yetu na wateja inahitaji kusubiri kama mwezi mmoja tu, tumeongea na mteja mmoja amekubali kuhamia popote hilo deni lake ili sisi tuuze na tuweze kupata hizo peta,, tafadhali kwa yeyote alie tayari atujulishe na tutamuachia faida ya kutosha kutoka kwa mkataba huo

Kwa msaada nenda pale brela waombe wakupe anwani za debt collection agencies watakupa na utasaidiwa kwa haraka kuliko kuwatafutia humu utaishia kudhalilishwa tu.au google kwa kuandika list of debt collection agency in Tanzania zinakuja kama kampuni tatu ambazo ni Zack finance,harvest Tanzania ltd na James Thomas makwinya advocate.
Nb.mkuu humu jamvini kuna watu wenye elimu tofauti usijekukuta ulikuwa unabishana na walimu,politician,sociolojia ukaumiza kichwa bure
 
Back
Top Bottom