Msaada wa kuuza hisa zangu!

Msaada wa kuuza hisa zangu!

UMUNYU

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2017
Posts
726
Reaction score
564
Naomba mwenye ujuzi wa taratibu za kufuata ili niuze hisa zangu naomba mwongozo!Mwaka 2013 nilinunua hisa za benki ya Mwalimu.Hadi leo hakuna kinachoendelea nimeishiwa kupewa tu risiti.Kila nikiuliza nakutana na "uswahili"uliosheheni na majibu yasiyoeleweka!Naombeni utaratibu wa kuuza hisa hizo ili nijitoe kabisa kwa hiyo benki!
 
Samahani ndugu, hebu funguka hapo Hisa ziko ngapi kwa sasa unazoziuza? Wewe uko wapi saivi? Na je, uko tayari kuuza kwa bei gani kwa sasa? Kumbuka Kwamba taarifa kama hizi na nyinginezo ndizo zinazoweza kutuvuta sisi wateja.
 
Fuata utaratibu uliotumika kununua hizo hisa. Mambo ya hisa tuachie tu wazungu ila sisi uswahili bado mwingi sana bora tuweke kwenye kibubu ni 100% safe.
 
Fuata utaratibu uliotumika kununua hizo hisa. Mambo ya hisa tuachie tu wazungu ila sisi uswahili bado mwingi sana bora tuweke kwenye kibubu ni 100% safe.
Ni utaratibu upi wa kufuata?
 
Ulinunua kupitia broker gani kama unaweza mtaje na idadi ya hisa zenyewe.. Kumbuka hivi tunavyoongea bei ya hisa moja sokoni ni 500
 
Uuzaji

Mwekezaji anayetaka kuuza hisa atafuata taratibu zifuatazo:

  1. Wasiliana na dalali wa soko la hisa na kumweleza kusudio lako la kuuza hisa
  2. Kabidhi hati yako ya umiliki wa hisa kwa dalali
  3. Dalali atahakiki umiliki wa hisa hizo kabla ya kuuza. Kama hisa haziko kwenye hifadhi ya hisa, dalali ataziweka kwenye hifadhi kabla ya kuuza
  4. Dalali ataweka oda yako ya kuuza hisa kwenye mfumo wa kompyuta wa soko la hisa akitumia namba maalum ya mteja. Iwapo bei unayotaka kuuzia hisa itafanana na bei ya mwekezaji mwingine anayetaka kununua, basi atakuwa amekuuzia hisa hizo na mwekezaji atalipwa.
Pia mwekezaji anaweza kununua au kuuza hisa kupitia mfumo wa simu ya mkononi kwa kupiga *150*36# na kisha kufuata maelekezo

Back
Top Bottom