Mimi ni Mtanzania nahitaji kibali kidogo cha uchimbaji madini ya dhahabu, nipo dar es salam ila naenda kuchimbia mahenge Morogoro so naombeni kupata mwongozo kibali hicho kinacost tsh ngapi hapa Dsm na eneo ambalo naenda kukikata.
Nenda ofisi ya madini iliyopo Upanga ukapewe maelekezo. Kimsingi ni lazima kwanza upate eneo la kuchimba ambalo liko wazi, yaani halina leseni nyingine. Baada ya kulipata eneo hilo, utatakiwa kupata coordinate zake. Utajaza fomu ya kuomba leseni iitwayo primary mining licence. Utaifikisha fomu hiyo kwenye ofisi husika, kwa upande wako utatakiwa kuipeleka ofisi ya madini morogoro. Utalipia ada iitwayo application fee tzs elfu hamsini. Baada ya maafisa hao kuridhika kuwa eneo liko wazi utalipia tena elfu hamsini ambayo ni processing fees. Leseni ikiandaliwa utatakiwa kulipa elfu themanini kwa kila hekta. Leseni moja inaweza kuwa na hekta zisizozidi kumi. Kwa maelezo zaidi tembelea website yao ya wizara Ministry of Energy and Minerals â The United Republic of Tanzania. Ndimi mbimbaji mwenzio.