Msaada Wa mada ya Sheria ngazi ya cheti

issakwisa6810

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2014
Posts
309
Reaction score
84
Naomba msaada wana jamiiforum kuhusu sehemu ya mada iitwayo criminal liability vire vineno vya actus reus and mens rea
 
Hizi ni kanuni za sheria za makosa ya jinai, kuwa kosa linahusisha dhamira (Mens rea) na kitendo halisi (Actus reus), katika tathmini ya kosa katika kesi, kanuni hizi ni sehemu muhimu ambayo mahakama itataka kujua na kujiridhisha kama zote zilitokea katika kosa husika.

maana yake ni hii, A amempiga kofi "B", ifahamike kuwa kitendo cha "A" kumpiga kofi "B" hakiwezi kuwa ni kosa moja kwa moja, sasa ili uweze kusema "A" ametenda kosa kwa kumpiga kofi "B" ni lazima ijiridhishe kuwa 1. kulikuwa na kitendo cha kumpiga kofi "B", na 2. "A" alikuwa na nia (Mens rea) ya kumpiga "B" na kumuumiza.

Hii ni kwa sababu, siyo kila anayempiga mtu kofi, anakuwa na dhamira ya kumpiga mtu kofi, wakati mwingine hutokea bahati mbaya kama vile mtu anavyokukanyaga, au anakuwa hayupo katika akili ya kawaida (temporary insanity)

Huu ni mfano tu, lakini mara nyingi kanuni hizi hutumika sana kwenye kesi za mauaji kutokana na uzito wa kesi, na hata adhabu itakayotolewa kwa mkosaji, huwezi kumuhukumu mtu kifungo cha maisha au kunyongwa kwa kosa ambalo alilifanya bila kudhamiria.
 
Asante sana
 
Katika makosa ya jinai huwa vinaangaliwa vitu viwli vikubwa ili kuthibitisha juu ya nti ametenda kosa hilo au la, navyo ni:

1. Kutendeka kwa kosa lenyewe (ACTUS REUS)

Actus reus is the latin maxim which means act, or physical act,
Mfano A amemuua B,, kile kitendo cha A kumuua B ni Actus reus yaan ni kitendo kimesha tokea

2. Nia ovu ya kutenda kosa hilo
(MENS REA)
Mens rea is also the latin phrase whc means the state mind

Akiwa na maan je wakat A ana muua B alikuwa kweng hali gan? Yaan akil yake ilikuwaje?

Ila kuna exception ya mens rea

Kwamba kuna baadh ya makosa ya kijinai wanaangalia tu kitendo bila kuthibitisha kipind unatenda hlo kosa state mind yako ilikuwaje,
 
name nikila point katik maswali ya kisheria kazima ujibu na kuambatanisha na kesi
 
Naomba msaada wana jamiiforum kuhusu sehemu ya mada iitwayo criminal liability vire vineno vya actus reus and mens rea
Actus reus means act itself and mens rea means mental. Kwenye criminal liability unatumia hvo vitu viwili kuprove kuwa mtu accused person. Actus reus unaangalia kitendo kilchofanywa na mtuhumiwa na mens rea unachek mtuhumiwa alikuwa anafikiri nn wakat wa kutenda kosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…