Msaada wa mapaa ya kisasa

mwilawi

Senior Member
Joined
Oct 13, 2013
Posts
139
Reaction score
89
Habari wadau, wataalamu wa mapaa tunaomba ufafanuzi na faida ya hiden roof na hasara zake kitaalamu zaidi. Na mfumo upi katika hiyo miwili ni mzuri na wenye tija kwa jengo.

 
Mfumo wa kwanza:

Faida:
Moja:Mbao ni kidogo sana unaweza kupunguza hadi 70% ya mbao ambazo ungetumia.

Mbili: Mabati ni machache sana kwasababu unayalaza tambarale katika mwinuko mdogo sana kama nyuzi 10° hivyo kufunika sehemu kubwa kulinganisha na kuyasimamisha katika nyuzi kati ya 30° na 45°.

Tatu: Misumari michache

Hasara:

Moja: ongezeko la uzito wa nyumba
(course za matofari) juu ya renta hivyo msingi lazima uende chini kuliko kawaida.

Pili: Kuongezeka kwa ujenzi wa vibaraza vya zege kukinga mvua kuingia moja kwa moja kwenye madirisha na pembeni ya ukuta wa nyumba hivyo ongezeko la gharama za ujenzi na muda.

Tatu: Ongezeko la ujenzi wa mifereji ya kukusanyia na kutoa juu ya paa maji ya mvua. Mifereji hii lazima ijengwe kwa ratio kali ya cement hivyo kuongeza gharama na muda.

Nne: Mabomba ya maji ya kutililisha kutoka kwenye paa hadi chini na ujenzi wa kingo za kuta kuyasupport ni ongezeko la gharama na muda.

Tano: Kuta za nje ya nyumba kulowa na kunywa maji ya mvua (japo mafundi usema wanapaka water proof) itapelekea mwenye nyumba lazima ufanyie ukarabati wa mara kwa mara kutokana na kuta kulowa maji ya mvua.

Sita: mwonekano wa nyumba hauvutii kama nyumba zinazopauliwa kwa mfumo namba 2.
Saba: Ongezeko la joto ndani ya nyumba kutokana na mzunguko mdogo wa hewa kwenye dari. Kitendo cha bati kuzilaza usawa wa ceiling board, joto la bati la jua upenya kirahisi kwenye (ceiling board) na hatimaye ndani ya nyumba tofauti na bati zilizoezekwa kwa kuinuliwa kwa nyuzi zaidi 15° ambapo uruhusu mzunguko mkubwa wa hewa kwenye dari kupunguza joto la bati la jua kupenya hadi ndani ya nyumba.

Hitimisho: Faida na hasara za upande mmoja ni hasara na faida za upande wa pili (respectively)
 
sijapenda kabisa hii type no 1

Sent using galaxy s10+
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…