Kwenye E-com development ina tengemea na wewe unataka iwe kwenye mfumo gani labda vitu vya msing kuzingatia ni
1.Front-back end development
hapa sasa zingatia front to back end ya web/app yako we rahisi kutumia kwa end user hapa najua utacheza na UI/UX
Ni kweli mkuu, nadhan nitatafuta kampuni yenye "reputation" katika utengenezaji wa responsive themes kwa ajili ya website yangu!!
2. Aina ya app/web
ume target wapi B2C, B2B , C2C au zote kwa pamoja??
Kwa kuanza nataka nianze mimi kama mimi, mfano nitanunua bidhaa either china au popote ambapo watakua na bei na quality nzuri then nitaanza kama sole seller wa site yangu, then nikipata uzoefu na challenges ndio nita scale kwa kuifanya multi vendor site ambapo wauzaji wengine watakuja kuuza!!
Nili focus sana kwenye B2C mostly yaani watu wanunue bidhaa kwa ajili ya matumizi yao! infact nitaweka pia mwanya wa B2B na C2C ila B2C ndio itakua lengo kuu!!
3. Fulfillment service
sasa hapa inategemea tena na je hizo bidhaa uta fulfill wewe au app yako itakua ina intergrate buyer & sallers kama kupatana?
Kama utakua una fulfill wewe system yako ya fulfillment warehouse ipoje kwenye ku-receive, storing, picking & packing??
Hii nayo ni moja ya challenges zinazo nipasua kichwa! as I said, kwa sasa nitaanza kama "online store" but at a time nikiscale ndio nita deal na hii challenge!!
Nilivutiwa sana na mfumo wa amazon FBA ambapo seller anapeleka bidhaa kwenye warehouse za amazon alafu amazon wanapokea order na kupelekea wateja, ni mfumo mzuri sana ila unahitaji heavy investiment kwa pesa na technology kitu ambacho kwahatua niliyo ni kigumu!
Kwa sasa seller atabaki na mzigo wake then order ikitokea basi yeye atautuma kwa mteja na huu mfumo unatumika hata na alibaba kuna option nyingine ambayo naweza kuwa napokea mzigo kutoka kwa seller order ikitokea alafu niwe natuma mimi ila challenge ya huu mfumo ni kwamba lets say niko mwanza alafu seller yuko dsm kidogo itakua ngumu! so seller ndiye atatuma mzigo na pesa atapata baada ya buyer kupokea na kuridhika na mzigo!!
5. Fake products and fake accounts
hapa ndo kuna shunguli ikiwa utatumia C2C umejipangaje ku deal na product feki zilizopo kwenye web yako unakuta mtu ameweka iphone 6+ kwenye bei ameweka 200,000 ki-ujumla huyu ni mwizi umejipangaje kuzuia. kama unauwelewa wa ku program AI ku detect fraud au fake account kwenye site yako ingekusaidia
Nitachofanya ni kila seller awe na mzigo wake, then mimi nitakua kama "escrow account" nitapokea pesa alafu nitaweka time interval ya kumlipa seller, mfano kwa wiki...sasa ndani ya muda huo kama buyer atakua na shida na seller akishindwa kutatua basi nitam refund pesa yake!!
Hii ni njia ambayo inatumika na paypal na njia rahisi ya kuhakikisha mzigo sio feki!!! infact nitaweka rules za kuhakikisha huu uhuni haupo!!
Hilo swala la AI japo sina ujuzi wa AI (na Machine learning pia) ila nitaliweka kwenye malengo yangu!!!
6. Who will handle returns
nimenunua bidhaa nimekuta imeharibika nairudisha wapi??
Swali zuri sana. Umefanya niwaze sana. Anyway kama nilivyosema hapo juu, mimi nitakua "escrow account" au nitakua napokea pesa alafu buyer akiridhika basi ndio nam fund seller pesa yake!! so niwajibu wake ajue kama akituma kitu feki basi ajiandae kwa gharama zitakazotekea kama hizo...
Najua kuna mengi yanaweza kutokea kama gari kupata ajali and the alike hayo nitayaangalia kwa undani muda huo!!
7. shopping cart
moyo wa e commerce ni shopping cart hapa unatumia software gani??
Sijui kama nitakua nimekujibu ila kwa sasa niko dillema either kutumia "magento" au "wordpress na woocommarce"!! either of them themes zake zinakua built in shopping cart zilitengenezwa kwa ajax kama sijakosea!!
Nashukuru kwa maswali yako, pia ningeomba mtazamo wako zaidi na mawazo kuhusu hili wazo kwa ujumla na kuhusu hizi platforms mbili ambazo zinanichanganyayaani magento na woocommarce, nilipplan niende na woocomarce hasa kutokana community yake sasa sijui maoni yako mkuu!!
Thanks once again!!