Msaada wa mawazo kuhusu tabia ya mwajiri wangu

mt2k2

Member
Joined
Feb 6, 2014
Posts
14
Reaction score
2
Poleni na majukumu ya kuelimishana. Mimi ni mgeni humu JF,nimepata msukumo kutokana na watu mbali mbali nilioona wanavyopata msaada humu JF
Mimi ni mfanyakazi wa Taasisi moja iliyo chini ya Serikali.na kutoka nimeajiriwa sasa haipungui miaka minne.
Mwajiri amekua akituhamasisha kusoma kila mara.Vile vile amekua akitukatisha tamaa kwa kutuambia tujilipie ada wenyewe.na tuombe likizo bila Malipo.Kutokana na kipato kidogo niliona vyema kuitikia wito wa kusoma ambapo mwaka jana nilipata chuo cha karibu na Maeneo ninayofanyia kazi chenye Masomo ya Jioni.Kutokana na kukosa pesa ya Ada kwa wakati ilinibidi kuahirisha mwaka.toka 2013/14 kwenda 2014/15.ili kujipanga kiuchumi.Cha kushangaza ni kua. Mwajiri ameamua kunihamishia sehemu ambayo haina chuo chochote muda mfupi kabla ya mwaka wa masomo kuanza huku akijua ninatarajia kuanza Masomo .Nilimwomba kwa barua asitishe ule uhamisho lakini amenipa majibu ambayo hayakuniridhisha.Ninaomba msaada wenu wana JF nifanyeje? .
 
hujasema ni kada gani ndugu hebu funguka zaidi
 
Mbona unaogopa namna hiyo?
Kwa vile umeamua kutoa ya moyoni basi toa bila woga la sivyo unaweza ukapata majibu yanayo endana na sredi yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…