msaada wa mawazo tafadhali...

msaada wa mawazo tafadhali...

shopping

Member
Joined
May 29, 2012
Posts
20
Reaction score
10
naomba kutanguliza samahani maana hili sio jukwaa lake lakin ni dharura...



mi na baadhi ya wenzangu tupo masomoni nje ya nchi, kuna mwenzetu mmoja ana tatizo, ni kwamba jina lililopo kwenye passport yake ni tofauti na majina ya kwenye vyeti vya form 4 & 6. hapa chuoni kafanyiwa usajili kulingana na majina yaliyopo kwenye vyeti vyake, lakni idara ya uhamiaji wamegoma kumpa kibali cha kuishi huku kutokana na majina yake kutofautiana, wao wanadai kwamba inabidi afanye usajili kulingana na majina yaliyopo kwenye vyeti ndo watampa kibali cha kuishi, lakini nadhani km akifanya hivi cheti chake cha mwisho kitatoka na jina hilo lililopo kwenye passport ambalo ni tofauti na vyeti vingine, hili litamletea shida baadae (kuwa na vyeti vyenye majina tofauti)...sasa wadau naomba ushauri wenu ili kuweza kumsaidia huyu mwenzetu, hapa kuna options mbili, aidha kukubali kuwa na vyeti vyenye majina tofauti au kubadili passport, suala ambalo ni gumu...



mchango wako ni muhimu sana lakini usitukane jamani..ahsanteni
 
Ungetoa mfano wa majina yakoja kama
Labda yeye passport ni XYZ na vyeti ni XMZ. Au? Maana haitoshelezi bila kuweka. Yalivyo unaweza tunga majina hata ukitaka tumia majina ya matunda kuonyeshea yalivyo. I hope umenielewa.

Ila kama ni togauti kabisa yaani ABC na XYZ duh???

Haya majina yamekaaje wataalamu waelewe vizuri.
 
Ungetoa mfano wa majina yakoja kama
Labda yeye passport ni XYZ na vyeti ni XMZ. Au? Maana haitoshelezi bila kuweka. Yalivyo unaweza tunga majina hata ukitaka tumia majina ya matunda kuonyeshea yalivyo. I hope umenielewa.

Ila kama ni togauti kabisa yaani ABC na XYZ duh???

Haya majina yamekaaje wataalamu waelewe vizuri.
majina yaliyoko kwenye vyeti ni John David Alex
majina ya kwenye passport ni John Alex Musa.

yani hapa kilichotokea ni hichi, yeye shuleni tangu primary school aliandikishwa kwa majina ambayo mawili ya kwanza yote ni majina yake(John & david) halafu linafuata jina la tatu ambalo ni la baba(Alex), hivyo vyeti yake vya Form 4 & 6 vinatumia jina la John David Alex.
alipokuwa anafuatilia passport alipoambiwa kuandika majina matatu, ndo akajiachanganya akaandika jina lake (John), jina la baba(Alex) na jina la babu(Musa), hvyo passport ikatoka na jina John Alex Musa.
 
Back
Top Bottom