Msaada wa mawazo ya Kisheria

maruudaniel

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2020
Posts
888
Reaction score
1,073
Katika kuajiriwa kwangu nimekutana na mengi magumu kupitia Manager niliyenaye kama miaka Saba hivi sasa ktk hii Kampuni.

Huyu manager alinipandisha daraja mwaka flani na kilichotakiwa baada ya kupandishiwa daraja ni kubadilishiwa Mshahara nilikaa muda kama miezi mitatu bila mabadiliko.

Ilinibidi nifuatilie documents alizonisainisha bila mafanikio kutoka kwake. Baada ya kuona hakuna mafanikio ilinbidi niombe maongezi kwa bosi wake ila kufanyika utekelezwaji kwa mabadiko ya mshahara.

Na tangu nilivyoanza kufuatia maslahi yangu huyu Manager amekuwa akinipa daraja baya na ktk haya madaraja mabaya amekuwa akinipa malalamiko yote amefika kwa Mwajiri kwa kipindi tofauti na haya malalamiko nimekuwa nikishinda cha ajabu mwajiri ameyaacha matatizo palepale pasipo utatuzi.

Je kama mwajiri amekuwa akikalia kimya swala mwajiriwa kuonewa na kuzulumiwa kwa muda mrefu kuna kosa kuishitaki Kampuni kwa huu uonevu na dhulma niliyofanyiwa kwa muda mrefu.

Kwa haya madai yote ushahidi wa maandishi upo kati yangu na Manager pamoja mwajiri upo. Na nimekuwa nafanyiwa visa vingi sana ili ifike mahali niache kazi ila nimekuwa mvumilivu sana kwa yote ninayokutana nayo.

Asanteni, sana na Mungu awaongoze ktk mawazo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…